TL. Marandu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 3,625
- 5,810
Kabla ya Kuendelea Niseme Tu, Siafiki Mada hii Kutumbukizwa na Kupoteswa Kwenye Mada yenye Ushauri Kwa rais ambayo haiko Mahususi Kwenye Swala Ninalolilenga. Moderators, Naomba Msiwe Mnakombine Mada tu kwa Vile kwenye Kichwa cha Habari Kuna Phrase za Kufanana. Nyingine Mnazokombine ni sawa na Inasaidia Zaidi. Lakini Nyingine Inapoteza Mada Nzima Katika Msitu wa Mawazo mchanganyiko. Kama tupo hapa Kujadili Demokrasi na Uwazi Kwenye Taifa, Tuonyeshe Mfano Hapa. Angalau Mtumie personal Alert mtoa mada kuwa Mada yake Inatarajiwa Kuunganishwa na Nyingine, Aiangalie kama kweli inaendana na Mada yake, Na Mwisho wa siku hata kama Mkiamua kuifuta kuiunga, iwe Kwamba Mmempa Fursa ya Kurespond. Nafikiri Ni Vizuri Kuonyesha Heshima Kwa Member wa JF, Kwani Kila Mmoja anamchango wake Kuifanya Kuwa na Sauti iliyo nayo Kwa Jamii.
NitaKuwa Mtu wa Hovyo Niikosoe Serikali yenye Maguvu ya Kutisha Ikikosea na Niogope au Nisite Kuwakosoa Mamoderator Wa JF, Wakikosea. Niliona Nilichomekee hilo Kwanza.
Sasa Mada Yangu:
Kuzuia Kuingizwa Sukari Kwa lengo la Kuamsha Uzalishaji wa Sukari Nchini, Pamoja na Kusaidia ajira na Kuinua Kipato cha Wakulima wa Miwa, Kwa asilimia 100% Lilikuwa Wazo zuri. Lakini Utekelezaji wake Ulikuwa Wenye kuleta matatizo ambayo hayakukusudiwa. Labda Nilaumu washauri wa Rais, Kwani Rais hawezi Kuachiwa Kila Kitu afanye mwenyewe,( unless alipewa Ushauri akaukataa au hakukaribisha ushauri) Mwisho atakosea au atafanya jambo bila kuzingatia mlolongo ambao Ni wataalamu wa swala husika tu wangeweza Kumsaidia. Na sio uchumi tu, Politic, National Security, Economic Planing, Budgeting, Foreign Policy etc.
Ushauri Wangu Ni Kuwa, Hili Swala la Sukari na Bidhaa Nyingine ambazo Rais anataka zizalishwe Tanzani. Hakuna haja ya Kutumia Misuli na Kusukumana. Sulihisho Ni Rahisi Mno. Serikali Ikopeshe Viwanda vya Sukari Mtaji wa Kuzalisha sukari nchini Mara mbili, tatu nne etc, Kulingana na Uwezo wa Viwanda na Malighafi ya Miwa. Kisha Baada ya Kutimiza hatua hiyo ya Kuzidisha Uzalishaji hapa Nchini. Hatua ifuate ya Kutoza Kodi Kubwa kupita kiasi, kwa sukari inayotoka nje ili bila kusukumana Wafanyabiashara waone hasara kuingiza sukari Kutoka Nje. Wanunue ambayo itakuwa kwa wakati huo inazalishwa nchini kwa wingi. Watu watapata ajira, Miwa ya Wakulima itanunuliwa. Viwanda vya Sukari Vitatengeneza faida. Vitaweza Kurudisha Mkopo, Vitaweza Kujenga Matawi mapya. Na mwishowe Kabisa baada ya Muda Sukari Kuingizwa Nchini itakuwa Ni Historia au Kiasi Kidogo sana. Linalofanyika sasa Ni Kuweka Gari La Kukototwa na Farasi na Kumshurutisha alisukume, tutakesha na Kuumizana sana! Na wala serikali isizuie wale wanaotaka kuagiza sukari nje, kama wapo tayari kulipa kodi 80% na waiuze kwa hasara ruksa!
Na Hili sio Kwa sukari Peke yake, Ifike wakati Tuache Kununua Silaha ndogo ndogo, Uniform, Viatu na sare za Majeshi yetu Kutoka nje. Hii itasaidia Ku Kutumia Raslimali zetu Kama Vile Ngozi, Chuma etc. Na Kuongeza ajira kwa Kasi. Lazima Tuanapokuwa na Miradi Mikubwa ya Ujenzi Tuweke Vipengele vya Mikataba ambayo itashawishi, Wakondorasi Kutumia Equipments Zinazotumia Natural Gas badala ya Diesel na Petroli. Hii itasaidia Kuokoa fedha za Kigeni na Pia Kupata soko la papo kwa papo la Gesi yetu. Lakini haya yote yanatakiwa Kufanywa kwa Hatua. Mfano, Nguo na Viatu vya Majeshi, Serikali Inaweza Kumtafuta Mzalendo ambaye Tayari anauwezo wa Kuendesha Kiwanda. Wakaingia nae Ubia kwa Kumpa Mtaji (Kwa Kumjilisha malengo) Kwa haraka Kiwanda cha Viatu vya Ubora Murua sana, Kinajengwa, Watu wanapata ajira, Wizara ya Ulinzi inaambiwa Mzabuni ambaye atapata Tenda ya Kusupply Uniform na Viatu vya Jeshi, Lazima alete Vya Made in Tanzania. (Baada ya Uzalishaji wa Uhakika kuwepo) Kama hataki basi tenda anapewa Mwingine. Na Baada ya Uzalishaji wa Kutosha, Wa Ubora wa Kutosha, Choice za Kutosha, then Tunaanza Kupandisha Ushuru wa Kuingiza Viatu Nchini.