'Mpambano' kati ya Ban Ki-moon na Moalem!

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
697
Reaction score
218
Umetokea ubishani mkali leo kati ya Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, na Waziri wa mambo ya Nje wa Syria Bw. Waled Moalem katika mkutano unaojadili Amani ya Syria nchini Uswisi ambapo Bw. Ki-moon alijaribu kukatisha hotuba ya Moalem kwa madai ya kutumia muda mrefu, lakini Waziri huyo akagoma na kushinikiza kuwa ni lazima amalize hotuba yake! Lakini baada ya mabishano ya muda, hatimaye walikubaliana Waziri huyo amalizie hotuba yake!! Haikuonyesha 'picha' nzuri kwa kweli wakubwa kubishana dunia nzima ikiona "live"!!

NB: Hata hivyo, muda rasmi wa hotuba ulikuwa ni dakika 7 lakini Moalem alitumia muda mwingi zaidi ya dakika 20!

Source: Aljazeera International ("Live" punde tu):
 
Ban Ki moon ni kituko kingne cha hii dunia ndio maana haishangazi yeye mwenyewe anaialika Iran halafu kesho yake Marekani anamwambia hawatakiwi kweli anawaondoa jamaa mjinga sana yule ni punga
 
Mualem alimtolea kali akamwambia Mr Ban you live in New York I live in Syria so i know what is going on in my country! Kimsingi Ban Ki moon hana ushawishi wowote pale UN kwani anajua fika Syria ni nchi ambayo IRAN inaicontrol kwa maana inaushawishi mkubwa kisiasa na kijeshi na ASSAD amedumu kwasababu ya Iran kwani kuna Hezboolah na revelutionary guards ambazo zinafundishwa na IRAN na kupewa vifaa vya kijeshi so kuiarika Iran then baadae kufosiwa na US ni jambo ambalo halina tija kwa kumaliza mgogoro wa syria...Na isitoshe Ban Ki moon ameshindwa ata kuwaonya US,SAUD,QATAR kwa kuwafund waasi ambao baadae wamegundulika kua ni alqaaeda ni jambo la aibu kwani yanayofanywa ni noma....So tutegemee huu mkutano wa GENEVA 2 hautakua na tija kwani IRAN bado ipo kidete na ASSAD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…