Inaonyesha waTz hamjui mlitendalo kama kushushua mtashushua mpaka mtachoka ,mtachezeshwa kwata kulia na kushoto na hakuna mabadiliko yeyote yale yatakayopatikana.
Hili linatokana na vyama vya upinzani kuogopa kuyavalia njuga masuala muhimu yahusuyo Katiba ya Nchi ,aidha tume ya Uchaguzi hivyo tuta na mtaendelea kila siku kusema hili na lile kumfichua huyu na yule inaonekana ni kama mnawaamsha waliolala na kuwafanya wazinduke na kutafuta njia nyingine .jiulizeni leo ni miaka mingapi mambo haya yamefichuliwa na ni muda gani yanapigwa danadana na mahakama na DPP ,je huku kupigwa danadana kutakwisha kwa siasa hizi anazoziendesha Sultani CCM si hasha hata Mwanakijiji anatumika katika kuwababaisha watu na wananchi kwa ujumla.
Ni lazima tutoke nje ya mstari huu uliopigwa wa kutodai mabadiliko ya Katiba na tume ya Uchaguzi leo bado miezi tu kuanza purukushani za uchaguzi nini kiandaliwe au kinaandaliwa na vyama vya upinzani kukabiliana na hila za Sultani CCM ,tujiulize hivi kusulubiana na mafisadi ndio njia itakayotukwamua ,maana Sultani CCM hutumia njia ingine kabisa ya kuyakwaa madaraka ya nchi hii ,Je njia hizo tunazielewa na kuzifanyia kazi ili kuziziba au tumefungwa kamba na kutulishwa nanga katika mafisadi na tupo tunahangaika nao hatujui hata hatma yao ,wakati hatima ya ushindi wa uchaguzi tunaijua ni kushindwa kwa hila kwa nini hatupiganii kuziondoa hila hizi tunabakia kwenye mstari wa mafisadi ,huku ni kuwekwa na jambo lingine ambalo linahusiana na utawala uliopo na si kwenye jambo ambalo litazaa matunda mazuri katika chaguzi zijazo ,tumewasikia wapinzani wakipiga mayowe kuhusiana na chaguzi ndogo ,Je wamefikia wapi ikiwa sasa tunahesabu miezi kuelekea uchaguzi Mkuu ? Amkeni na ondokaneni na kikao cha mafisadi hapo ni mgandisho tu hakuna natija nzuri kukabiliana na matokeo ya Uchaguzi.