Moyo una mazito

Moyo una mazito

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,042
Reaction score
1,308
Mimi ingawa sisemi

Utasema ninaringa, njiani nikikupita
Mawazo yakinitinga, huenda nikabubuta
Majambo nikiyapanga,nikenda kwa kujivuta
Mimi ingawa sisemi , ila ninayo mazito

Utazani nina njaa, ninavyoinywa kahawa
Hunipoza na ajaa, kichwa kikielemewa
Usije ukashangaa, nikiwapo nimelewa
Mimi ingawa sisemi , ila ninayo mazito

Mara nahisi abiri, kumbe nipo nchi kavu
Upendo nikihitari, wanitupa kuti kavu
Hayo mambo ya dinari, yanitoa ushupavu
Mimi ingawa sisemi , ila ninayo mazito

Hivyo nanyi mubaini, naugulia kwa ndani
Si kwamba naona shoni, ndo mazito duniani
Ninawahi kilabuni, kupoza yalo kitwani
Mimi ingawa sisemi , ila ninayo mazito

✍️ Abuuabdillah
 
Back
Top Bottom