Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,790
Mwanasiasa Mkongwe Zanzibar, Hassan Nassor Moyo, amesema mgogoro wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar hauwezi kumalizwa kwa kurudiwa, badala yake ukamilishwe wa Oktoba 25, mwaka jana na mshindi wa urais, atangazwe.
Imekuwa jambo la kawaida na la aibu kwa C C M Zanzibar kuwa chama cha kulalamika tu, pamoja na kunasibu kuwa ndio chama tawala.
Itakumbukwa hata pale weananchi wa Zanzibar walipopiga kura ya maoni kuhusu serikali ya kitaifa, wazanzibari 66% waliunga mkono SUK na hivyo kuundwa kinyume na matakwa ya CCM ambayo mawazo yao yalisambaratishwa.
Baada ya muda wakaanza kulalamika kuwa kura ya maoni ilipigwa kwa hila ndio yakaja matokeo hayo. Kichapo kitakatifu cha Oktoba 25 CCM imerejea nyimbo ileile kuwa uchaguzi haukuwa huru.
Kabla ya hapo ZBC kulikuwa na tangazo la uchaguzi likimuonesha Dr. Shein akisema " uchaguzi wa mwaka huu utakuwa huru na wa haki, na nakwambieni tena mchana, kweupe, maana wakishindwa wanasema kura zetu mme tuubia...meetuibia".Kidokezo kama hicho kinatiliwa mkazo na Mhe. SEIF iDD kwa kusema "kila siku mnaibiwa nyie tu kura... basi nyie wapumbavu"
Leo hawaoni hata aibu ya kusimama na kulia " uchaguzi haukuwa huru na haki"
Uchaguzi wa wachovu ( walioshindwa) utafanyika tarehe 20 Machi 2016 , Sote twendeni tuakawape moyo, tukiwaangalia matori wakishindana wenyewe kwa wenyewe