Movie hii ni kichefuchefu!!!

Haters.
Mtu badala ya kushauri mnaponda tu, sasa si mseme wafanyeje ili waboreshe?
 
Haters.
Mtu badala ya kushauri mnaponda tu, sasa si mseme wafanyeje ili waboreshe?

washafundishwa saana,wakati mwngine adi wapondwe ndo watabadilika,inaonesha we ndo muvi zako hizi!
 
As much as nninavopenda kutukuza vya kwetu! Bongo movies zimenishinda kabisa hiyo uliyosema sijaiona ila sidhani kama itaifikia ubaya movie moja inaitwa saradini worst movie ever!
 
Jamani kwa nini msitoe alternative solution wote mnapondea kazi za watanzania wenzenu? Kwa hali hii hatutakaa tuendelee.
 
Nawahakikishieni kuwa Bongo movie haitobadilika ikiwa sisi tunaolaumu hatutachukua hatua yoyote. Angalau katika watu wote waliochangia thread hii basi wapatikane watano tu wafanyie kazi kasoro zilizopo. Mimi naanza.
 
Ikifikia. Mtu anataka afundishwe hadi kujijua yeye ni nani,ujue ana tatizo lisilo na ufumbuzi wa haraka!ni sawa na mtu alijisaidia pembeni ya choo na kisha kuomba aonyeshwe tundu baadaye,,kwa nini wasijifunze kikamilifu kabla ya kuvamia fani hiyo?nimezipiga marufuku kwangu,huo uzungu wao wa kizaramo siutaki,waniharibie watoto wangu halafu nisiwaponde?staki kuzisikia kabisa.
 
Tatizo kila Bishoo na Sista duu anataka kutoka kupitia Muvi. Bora nikaangalie kamata mwizi men, Wasanii Bongo hawataki kujifunza na kusikiliza ushauri wa bure,,,,!!!
 
Je ulishaona hata siku msanii wa Bongo anafanya tathmini ya Kazi yake hadharani na kuomba Ushauri wa wapi arekebishe na wapi aboreshe, Watu hawapondi ila wanazungumzia ukweli juu ya kazi za wasanii wetu,
Jamani kwa nini msitoe alternative solution wote mnapondea kazi za watanzania wenzenu? Kwa hali hii hatutakaa tuendelee.
 
hata mimi jamani sifagirii movie hizi za kibongo, nikiangalia tu lazima nisinzie!! na hasa mi-part II yao!
 

Hiyo business ipo kwa ajili ya kutangaza biashara hasa2 kwa wasichana na wanaume nao wanapata mademu kiurahisi
mitaani lakini si kwa ajili ya burudani wala mafunzo! yaani ni usanii hasa !!
 

Na siku ukipata bahati ya kuona filamu nzuri ya Kibongo uje kutuambia pia...
Pia, angalau maoni yako kwa filamu yachambue kwa kina kwa kutueleza sehemu zipi wamefanikiwa na sehemu zipi wamechemsha, kuliko kuponda tu! Tuone na sisi tuna jukumu la kuwasaidia kufanya kazi nzuri.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…