Ndugu Wanajamii Wasomi na Wasiowasomi,Salam,
Mimi kwa hili lakuhitaji Katiba Mpya naliunga Mkono mia kwa mia,Lakini tatizo langu kwa wasomi wengi hapa Tanzania ni waoga sana,Kwa upande mwingine wapo upande wa Serikali,ndio maana wanashindwa kutoa maoni na mwongozo wa jinsi ya kuunda Katiba.Kwa nini ninasema hivyo hawa jamaa muda wao mwingi wanakua katika kuandika machapisho mbali mbali,kwa hiyo nilidhani hawa wangekuwa mstari wa mbele kudai Katiba mpya,lakini hoja ya katiba mpya ilitoka kwa vyama vya upinzani,baada ya kushiriki kwenye chaguzi mbali mbali na kugundua kuwa kushindwa kwao tatizo ni Katiba,napenda kuuliza hawa Wasomi walikuwa hawalioni hilo siku zote,au ni woga wa kupoteza ajira,Ninasema sio wasomi wote waoga,lakini wengi wetu tunaogopa vyombo vya dola hata katika kutoa hoja zetu.
Kwa hiyo hawa wasomi wanatakiwa wakatoe elimu ya uraia kule vijijini na sio tu kujificha kwenye makongamano kwenye vyuo vikuu,Na kama utakumbuka hawa wanachuo hata mwaka jana kwenye uchaguzi mkuu hawakupiga kura,Na waalimu wao hawa kuwatetea,kuwa ile ilikuwa ni haki yao ya Kikatiba,Mimi hili linanipa wasiwasi juu ya Wasomi wetu,Mimi kwa uelewa wangu Chuo Kikuu ni Sehemu huru ya kutoa mawazo,kukosoa serikali,kuishauri kwa kupitia tafiti ambazo zina majibu yaliyofanyiwa uchambuzi wa kisayansi.Na kuwaelimisha wananchi wa vijijini ambao hata hawajawahi kuiona Katiba licha ya Kuisoma,waulize ni wanachuo wangapi waliokuwa wanajua Katiba Miaka kumi nyuma kabla ya Hoja hii kuingia.Kwa hiyo ni makundi yote yanatakiwa kudai katiba Mpya.
Lakini kuna Makundi yanatakiwa kuongoza umma na kuuelimisha,Wenzetu Kenya walienda kuelimisha wananchi Kaya hadi kaya.Na sio kujicha kwenye vioyoyozi eti unadai Katiba.No easy Tasks by Nelson Mandela.