Move on!!

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,711
Haitajalisha ni kwa kiasi gani unajisikia vibaya. Ni muda wako sasa wa kuacha kumfikiria huyo anayeupiga danadana moyo wako na kukuchukulia poa, mtu ambaye ameshindwa kabisa kuthamini na kumjali kwako, kumpenda kwako na kujitoa kwake.
.
Hauwezi kuendelea kukaa huku ukiumia. Haiwezekani uendelee kutoa machozi juu ya mtu ambaye hastahili tena moyo wako.
.
Hauwezi kujisikia hatia kwamba umeshindwa kupigania mahusiano yako wakati ni wewe peke yako unayehangaika.
.
Hauwezi kumfanya akupende kwasababu kama angekuwa amekupenda asingekuumiza kila siku. Unastahili kilicho bora. Unahitaji mtu ambae atathamini hisia zako na ambaye hatakuletea michezo ya kitoto.
.
Ni kama vile kidonda kikubwa katika kidole chako kinavyokawia kupona, moyo wako pia unahitaji muda kupona.
.
Unaumia na mahusiano? Sio muda wa kuona kama Dunia imekutupa. Utapona maumivu yako na siku moja utakua ubavuni kwa mtu anayekupenda kinyama.
.
It can only be true love when you enable your other half to be better, to be the person they're destined to be.
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…