Kwa mara nyingine tena katika hali inayo onekana ya kutaka kuleta machafuko hapa nchini kwetu,leo huko mkoani TANGA kaibuka kijana wa ki-islam alie kojolea BIBLIA kwa kile kinacho onekana kulipiza kisasi kufuatia kisa cha yule kijana wa mbagala aliefanya jaribio la kuthibitisha kama kukojolea MSAHAFU hakuwezi kumfanya mtu ageuke kuwa NYOKA,jaribio hili lilifanywa na kijana(mtoto) huyo baada ya kuletewa kitabu hicho na kijana(mtoto)mwenzie kuja na kitabu hicho na kubishana kwa suala hilo la mabadiliko ya ki-maumbo.
** * Huyu wa leo yeye hajaletewa na mtu,wala hapakuwa na mabishano kuhusu kitabu hicho kitakatifu kwa waumini wa ki-kristo ila tu kwa kuwa kile cha waumini wa ki-islam QURAN tukufu kilikojolewa basi nae kaamua KURUDIA ATUKIO KAMA LILE.
chanzo cha habari hizo kinatonya kwamba viongozi wa ki-kristo wameripo pia jambo hilo kuambatana na uchomwaji wa makanisa matau(3)na WAISLAM hapo mjini Tanga,
* * Habari hiyo ilizidi kujuza kuwa imeonekana kuwaJESHI la POLISI limefumbia macho suala hilo kwani mpaka vyanzo hivyo vinakwenda hewani usiku huu hakuna mtu YEYOTE aliechukuliwa hatua za kisheria mbali na watu hao kujulikana kwenye jamii husika.
* * * maswali ya kujiuliza/kuwauliza jeshi la polisi:
1/:Jeshi la POLISI mbona mnajishushia UWELEDI wenu?,
*2/:mnataka mpaka hali iwe mbaya ndo mjae mabarabarani mkisaidiana na jeshi la wananchi KUFUJA,KUPOTEZA MUDA NA NGUVU bila sababu za msingi?
*3/:Au mnahamu ya kutumia tena hayo mabomu yenu ya machozi?,kama jibu NI hapana mbona hamshughuliki na huu moshi kabla mioto na milipuko haijatokea?
USHAURI:Ni vema jeshi la polisi mkachukua hatua za kuzima ujinga na upumbavu huu kabla haujaleta madhara na mtafaruku kwa jamii. wenye akili finyu kama hii ya kulipiza KOSA Kwa kufanya kosa bado wapo wengi kwenye jamii yetu ambayo bado ina pambana na ma adui wa tatu yaani maradhi umaskini na UJINGA,tena hili la UJINGA hapa naona LIMECHIPUA kuelekea UPUMBAVU.
*MWISHO vijana (Watoto) wafundishwe ukweli kuhusu KUHESHIMU vitabu vya dini na sio kuwafundisha U-ONGO badala yake wanazua mabishano kama haya ambayo baadae yanaleta shida kwa taifa.)
*
source: RADIO1