kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,120
- 24,395
Katika hali isiyokua ya kawaida mama mmoja mkazi wa kijiji cha Kimira Masama Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro anayefahamika kama "Mama Asha" ameuliwa na kuchinjwa na kijana wake wa kiume
Inadaiwa kuwa kijana huyo alikua haishi hapo nyumbani kwa mama huyo
Inadaiwa majuzi tu baada ya mama alitoka msikitini kisha akaelekea nyumbani kuandaa futari
Inaelezwa kuwa wakati anafutari akiwa dukani kwake ndipo mwanae huyo alikuja nyumbani ghafla akaingia dukani na kumvamia mama yake huyo na kisha kuanza kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Jirani mmoja aliyekua anakatiza katika eneo hilo alipoona tukio hilo alipiga mayowe huku kijana huyo akafanikiwa kutoroka na kukimbilia kwasadala.
Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
UPDATE ZAIDI
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Safina Tarimo (78) amefariki dunia katika tukio la kusikitisha lililotokea katika Kijiji cha Kimira, Kitongoji cha Majengo, Kata ya Romu, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro baada ya mtoto wake wa kiume Jumaa Ramadhani (40) kumkatakata kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo .
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa eneo hilo, marehemu alikutwa amefariki ndani ya nyumba yake Machi 2,2026 huku damu ikiwa imetapakaa eneo lake la kazi alipokuwa akifanya biashara ya kuuza duka.
Mashuhuda wameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya Kijana huyo kumtuhumu mama na ndugu zake kuwa ni wachawi na wamekuwa wakimroga ili asifanikiwe ambapo alifunga safari kutoka Kwasadala anapoishi na kuja kutekeleza unyama huo huku akiwa ameficha sura.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (SACP) Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa ametafutwa mara kadhaa nyumbani kwake bila kupatikana hivyo Jeshi la Polisi bado linaendelea kumtafuta ili hatua za kisheria zichukuliwe .
Mwandishi @mc_malaika_event
@nuhu_suleimantz