Kwa wale ambao ni wapenzi wa filamu za Magharibi, bila shaka jina Morris Chestnut si geni katika fikra zenu...
Mwenye picha hiyo hapo juuu haswa ndiye kijana Morris na mmoja kati ya wasanii wenye kipaji cha hali ya juu katika uigizaji miongoni mwa Waamerika wenye asili ya Kiafrika...
Binafsi nimekuwa nikijikita kwenye tafiti zangu binafsi, tafiti ambazo zitanifanya na hunifanya kuwaelewa wanawake katika angles tofauti.
Kwenye moja ya tafiti zangu nimegundua kuwa wadada/wanawake wengi ambao ni wapenzi wa filamu, huvutiwa sana na huyo bwana hapo juu. Yaani kuvutiwa kwao ni kwa kimahaba zaidi na wala si sanaa aioneshayo.
Wapo waliodiriki/wanaodiriki kusema kuwa kama kungelikuwa na nafasi ya kulala na huyo jamaa basi hilo zoezi wala lisingelikuwa na ukinzani wowote.
Sasa naomba niwaulize ninyi wadada/wanawake...Kwa nini mnampenda/mnamzimikia sana Morris?
Ni kitu gani ambacho kwake huwa mnakiona na hakionekani kwa wanaume wengine?
Ni vitu gani ambavyo huwa ukiviona kwa mwanume(hapa namaanisha mwanaume yoyote), huwa vinaukuna mtima wako kiasi cha kumtamani hata kwa "a single one night stand"?