Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Chama cha demokrasiana na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Morogoro kimekusudia kuliburuza Mahakamani Jeshi la Polisi wilayani humo kupinga hatua ya jeshi hilo kukinyima uhuru wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata ya kiwanja cha ndege kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwakamata hovyo wanachama wa Chadema.
Akitoa tarifa kwa vyombo vya habari katibu wa Chadema mkoa wa Morogoro Bwana.Samwel Kitwika amesema chama kimefikia uamuzi huo kufuatia jeshi hilo kuonekana kuegemea upande mmoja wa chama huku akiitaka tume ya taifa ya uchaguzi kusimamia kwa uhuru na haki uchaguzi huo.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Devota Minja amewataka wananchi wa kata ya kiwanja cha ndege kuwa watulivu wakati wakijiandaa kuchagua kiongozi atakayewaongoza kwa manufaa ya wakazi wote wa kata hiyo.
Chanzo: ITV