Morocco yatamani kurejea Umoja wa Afrika

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Morocco imetoa tamko la nia yake ya kutaka kujiunga tena katika umoja wa Afrika.

Katika ujumbe uliotumwa kutoka kwenye mkutano wa Umoja wa Matataifa ,mjini Kigali, Rwanda, Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita amesema sasa ni wakati muafaka kwa taifa lake kurejea na kuchukua nafasi yake katika jumuiya hiyo ya umoja wa Afrika.

Morocco ilijitoa katika umoja huo mwaka 1984 wakati umoja huo ulipotambua uhuru wa eneo la magharibi mwa sahara.

Morocco ilidai kuwa eneo la Magharibi mwa Sahara lilikuwa ndani ya mipaka yake.

Hata hivyo Umoja wa Afrika umesema utaendelea kusukuma upatikanaji wa haki ya watu wa eneo la Magharibi mwa Sahara ili kuwa na uhuru kamili bila kuingiliwa

Chanzo: BBC
 
Anakosa nini kwa kuwa nje ya genge la madikiteita wa kiafrika?
 
Morocco awali Ilikuwa mwanachama wa Umoja wa Afrika lakini aliondoka mara baada ya Sahara Magharibi ilipokubaliwa uanachama wa Africa na OAU. Hii ni kwa sababu Morocco Iliitambua Sahara Magharibi kama sehemu yake, Hivyo kwa lugha nyingine, tunaweza kusema "waliaamua kususa..." Issue ya kujiuliza, je zile sababu zilizowafanya waondoke zimeshaisha? wawakazie tu....kwanza ni Magaidi...
 
Back
Top Bottom