Monduli: Mwanafunzi wa Sekondari ajifungulia bwenini

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Ni katika shule ya Sekondari ya bweni ya wasichana ya Irkisongo iliyopo wilayani Monduli ambapo mwanafunzi wa kidato cha nne amejifungua mtoto wa kike majira ya saa mbili usiku wa jana wakati wenzake wanajisomea madarasani.

Habari zaidi zinasema mara baada ya kujifungua, mwanafunzi huyo na baby wake walihamishiwa katika hospitali ya wilaya Monduli hadi sasa.Habari zaidi za kushangaza ni kuwa mwanafunzi huyo jana aliingia darasani kama kawaida.
 
Pole sana binti hayo yametokea kutokana na hali hivyo umejikaza mpaka dakika ya mwisho. Mzazi mchukue kichanga mrudishe binti shuleni amalizie masomo kwani ndio mkombozi pekee aliyebaki!
 
matron wa bweni hilo ni jipu, please lowaxa li2mbue
 
duu,, sishangai coz hata sisi lishawai kutokea chuo,, Mdada kaJifungua saa 11:30 asuBuhi saa8:00 tukaMwona kwenye Mtihani,, tena yupo norMal kaBisa,,!
 
Ni katika shule ya Sekondari ya bweni ya wasichana ya Irkisongo iliyopo wilayani Monduli ambapo mwanafunzi wa kidato cha nne amejifungua mtoto wa kike majira ya saa mbili usiku wa jana wakati wenzake wanajisomea madarasani.

Habari zaidi zinasema mara baada ya kujifungua, mwanafunzi huyo na baby wake walihamishiwa katika hospitali ya wilaya Monduli hadi sasa.Habari zaidi za kushangaza ni kuwa mwanafunzi huyo jana aliingia darasani kama kawaida.
SAFI SANA, INATAKIWA AKAE MATENITE THEN AENDELEE NA SHULE.
 
HONGERA kwa kujifungua salama na kutotoa mimba ila kwann msisubiri wakati wenu? sampuli za wanafunzi kama hawa ndio wanawafundisha tabia mbaya wanafunzi wengine

niwape siri wanafunzi wengine mkimaliza shule mta sex mpaka watajionea wanazeeka na kupunguza dozi maana wanaume wenye makamo hupenda vibinti ila kwa sasa huyu anayependa fasta anaweza akawa amejitia dosari kwa kua na mtt na akashindwa kuyafaid maisha ya mapenzi na pia kumkosesha mapenzi sahihi mtt wake

kila kitu kina wasaa wake na utafaidi zaid ukikifanya kwa wasaa
 
Hapa kazi tu ndo kwanza imeaza. ongera yake kwa kuonyesha ujasiri wa hali ya juu na kutia bidii kwenye masomo
 
Tatizo liko wapi mwanfunzi kujifungulia bwenini kwani mimba ni ugonjwa ?? ,tena inabidi tuangalie upya hili swala ili kuwapa haki stahiki hawa watoto wa kike wanao onekana ni mizigo kwenye jamii zetu ,Dunia inabadilika sana na changamoto nyingi mpya zinatokea ,kumfukuza mtoto shule kisa kabeba mimba naona ni uonevu ,angekua hana uwezo wa kushika hiyo mimba asinge beba mimba kwa maana hiyo mwili wake ulikua tayari kabisa kwa shughuli hiyo na hapa nisieleweke vibaya ,haina maana natetea mwanafunzi kubeba mimba ila linapotokea hivyo basi tutatue tatizo katika muelekeo chanya
 
Duh, huyo mwanamke wa shoka. hongera zake. Nimejifunza kitu apa, wanawake wa mjini wanadeka sana.
Haha uchungu unatofautiana
kila mmoja ana hatua fulani tofauti na mwingine
wapo watu hujifungua vizuri mtoto wa kwanza lakini wapili ikawa ngumu
 
Back
Top Bottom