Tukielekea kwenye maadhimisho ya siku ya mama Duniani tujaribu kurudi nyuma na kujikumbusha juu ya matukio au mambo muhimu ambayo mama zetu wametundea na kuleta Matokeo chanya kwenye maisha yetu.
Nakumbuka siku moja wakati nikiwa kidato cha pili nimerudi nyumbani likizo fupi ya pasaka. Nilipofika nyumbani niliuliza mama yuko wapi? Dada zangu walinijibu yuko porini. Anafanya nini? Nikajibiwa anauza pombe (ya kienyeji). Kwanini anauzia porini?
Kwasababu ya karantini ya kipindupindu, pombe imekatazwa kuuzwa kuogopa kusambaza maradhi ya kipindupindu. Daa, niliishiwa nguvu na kuingiwa na huruma sana kuwa mama yangu anavunja sheria kwa sababu ya mapenzi yake kwangu kwakuwa asipouza pombe mimi sitapata ada na sintakwenda shule. Sikukaa chini, nilikwenda kumtafuta mama yangu.
Nilipofika huko porini, nilimuona mamangu akiwa katikati ya kundi la wanywaji akichota pombe kutoka kwenye pipa na akitia kwenye sadolini na kuuza kwa wanywaji. Roho iliniuma sana, machozi yakanitoka. Nikaenda kumwamkia, nikambusu na nikaanza kumsaidia kufanya kazi ile ingawa alinisihi sana niende nyumbani lakini sikukubali hadi tulipomaliza, nikamsaidia kuosha mapipa na vyombo vingine vilivyotumika. Tulipofika nyumbani, baada ya mahesabu yake Mama aliniita chumbani kwake na kunipatia pesa ya ada na matumizi yangu ya shule na hapo mchozi ulinitoka tena.
Kwa ufupi mimi nimetoka familia masikini yenye kulelewa na mama tu, nilisoma shule za kawaida za Serikali nikienda shule bila hata kandambili. Juhudi za Mama yangu kipenzi za kuuza pombe ya kienyeji na kulima kilimo cha kimasikini ziliniwezesha mimi kuwa hapa nilipo.
Leo hii mimi ni miongoni mwa watu waliofanikiwa kimaisha katika maeneo mengi, nimesoma vizuri na nina Master degrees tatu za fani tofauti kutoka vyuo vinavyoheshimika Duniani, nafanya kazi na miongoni mwa mashirika makubwa na linaloheshimika sana duniani kwa takribani miaka kumi na tano hadi sasa nikifanyakazi nchi mbalimbali Duniani. Bahati mbaya zaidi kipindi hiki ambacho Mama yangu alipaswa ale matunda yangu, Mungu alimpenda zaidi kuliko mimi na aliamua kumchukua.
Sina chakumpa Bi Mkubwa yule bali ni kumuombea kwa Allah amsamehe dhambi zake za kibinadamu na amlaze pahala pema panapostahili Peponi. Amen. Angalizi, mlio na mama zenu hai, Watunzeni mama zenu pasi na kulalamika kuwa kwanini wewe tu wakati watoto mko wengi, kila mtu anafadhila zake kwa mamake na msiwachoke kina mama hao kwani wao hawakutuchoka hata dakika moja ya maisha yetu walijitoa muhanga kwa ajili yetu.
Sisi wenzenu tunalilia laiti mama zetu wangekuwa hai ili tuwape kila wanachohitaji. Asante mama, nakupenda sana na sitakusahau mpaka naingia kaburini. Na kutokana na wewe, nawaheshimu sana wanawake wote Dunuani na hasa wanawake waliodhalili.
NAJIVUNIA MAFANIKIO NILIYONAYO LEO KWA SABABU YAKE YEYE, ASANTE MAMA