MOI kuendesha Kliniki Maalum katika Maonesho ya Sabasaba 2025

MOI kuendesha Kliniki Maalum katika Maonesho ya Sabasaba 2025

Joined
Apr 15, 2025
Posts
91
Reaction score
174
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inatarajia kuendesha kliniki maalum ya kibobezi ya matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba kwa mwaka 2025.

Hayo yalisemwa Juni 27, 2025 na Meneji Uhusiano wa MOI, Bw. Patrick Mvungi katika mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika taasisi hiyo.

Bw. Mvungi alisema Taasisi ya MOI itashiriki maonesho hayo kwa namna ya tofauti na miaka mingine ambapo madaktari bingwa wabobezi wataendesha kliniki maalum ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

"Tutakuwa na kiliniki maalum ya madaktari bingwa wabobezi wa mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, ambapo wananchi watahudumiwa pale kwenye Viwanja vya Sabasaba" alisema Bw. Mvungi na kuongezea

"Tofauti na miaka mingine ambapo tulikuwa tukionesha huduma zetu tunazozitoa MOI tumeona ni vyema kuzisogeza huduma zetu kwa wananchi"

Pia, Bw. Mvungi alisema kuwa gharama ya kumuona daktari bingwa itakuwa shilingi elfu tano (5,000) na kipimo cha ultra sound kitakuwa elfu kumi (10,000).

Kwa upande wake, Daktari bingwa mbobezi wa upasuaji wa mifupa MOI, Dkt. Tumaini Minja alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo adhimu kufika katika banda namba 12 la MOI kwa ajili ya kupata huduma hizo za kibingwa .

Pamoja na mambo mengine Dkt. Minja alisema kutakuwa na madarasa maalum ya lishe bora ambapo wananchi watapewa elimu bure kuhusu lishe bora.

Pia, Dkt. Minja alisema MOI itatoa elimu na huduma za mazoezi tiba kwa wananchi ikiwa ni pamoja na mafunzo ya mitindo bora ya maisha ili kujiepusha na maumivu makali ya mgongo ambayo ni changamoto kwa watu wengi.
IMG-20250627-WA0046.jpg
IMG-20250627-WA0045.jpg
 
Safi sana, vipi kama mtu anatumuia bima hawezi kupatiwa huduma kwa hapo?

Na kama bima inatumika ni bima zipi zitahusika kwenye hilo zoezi hapo sababa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom