Mogella, pawasa wawafunda wachezaji wa simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mogella, pawasa wawafunda wachezaji wa simba

Discussion in 'Sports' started by KIM KARDASH, Mar 6, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Habari na picha kwa hisani ya mamapipiro blog..

  [​IMG]
  WACHEZAJI wa zamani waliopata kuichezea timu ya soka ya Simba, Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy' (kushoto) na Boniface Pawasa wamewaasa wachezaji wa timu hiyo kuichezea timu hiyo kwa nguvu zote ili kuiletea mafanikio.
  Wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Simba Tv mwishoni mwa wiki iliyopita, Mogela na Pawasa walisema mafanikio ya Simba yatapatikana kutokana na kujituma kwao.Walisema kutokana na timu hiyo kuwa na kila kitu ikiwemo kocha mzuri pamoja na wachezaji wenye vipaji hawana budi kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vema katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.
  "Nakumbuka wakati ninaichezea Simba miaka ya nyuma kikubwa ilikuwa ni kutanguliza utashi wa kazi yangu hii pamoja na maslahi ya klabu kwanza na ndipo mafaniko yalipatikana, hivyo nawaomba wadogo zangu mtangulize maslahi ya Simba kwanza ili muweze kuwa na mafanikio,"Alisema Mogella.
  Mogella alisema kwamba macho na akili za mashabiki wa Simba zipo mikononi mwao hivyo kufanya kwao vibaya kutawaangusha pia Wanasimba wote na Taifa kwa ujumla.
  Naye Pawasa aambaye alipataa kuicheze timu hiyo katika miaka ya mwanzo mwa 2000 hadi 2005 alisema enzi zao walikuwana kauli mbiu ya ‘Simba Kwanza' na kutokana na hilo waliweza kupata mafanikio.
  Akiwa ni mmoja ya wachezaji wa Simba walioweza kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri mwaka 2003, alisema anaaminani na timu hiyo kuweza kufika mbali katika michuano ya kimataifa kutokanba na vipaji walivyonavyo lakini kikubwa zaidi ni wachezaji wake kujituma.
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Namkubali morgan,hakujawahi tokea mpachika mabao kama yeye toka aondoke kwenye mpira kidogo marehemu said mwamba "kizota" alitaka kumkaribia kabla ya kubadilisha namba na kuwa beki wa kati katika siku zake za mwisho mwisho katika soka na kwenye maisha pia.
   
Loading...