Modem inanizingua

BILGERT

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2015
Posts
6,533
Reaction score
11,027
Msaada wenu wakuu,modem yangu hupatwa na matatizo ya ku fail nnapo taka ku connect data.inaniletea ujumbe ambao nmescreen na ku attach hapo chini.huwa nna un install,halaf nna install tena,hapo itaendelea na kazi kama kawaida.ila tatizo hujirudia tena mara kwa mara.hvo inanibid nifanye kazi ya ku unistall na ku install tena.

Naomba msaada wenu wadau,ili hili tatizo liweze kufumbuliwa moja kwa moja bila kujirudia.



note.
Natumia modem ya airtel ila ni multi purpose
View attachment 554143 View attachment 554144
 
mara nyingi ni driver conflict mkuu, ndio maana ukitoa ukieka inakubali then badae inakataa.

jaribu kutoa dashboard zote zisizo na maana nenda na device manager un install modem zote halafu eka upya dashboard yako na driver za hio modem maisha yaendelee
 
Mkuu jaribu huo ushauri wa chief
 
Hakikisha Windows 10, operating system unayotumia kufuatana na hiyo picha inaona drivers za hiyo modem yako. Siyo kila operating system hizi modem zinaweza kufanya kazi. Angalia operating system specifications ya hiyo modem yako.
 

Shukrani kwa ushauri wako mkuu.ila sorry,mimi sio mjuz wa computer na program zake,ni mtumiaji tu.maana hata juzi kati ilizingua,ile sehemu ya ku connect,ikawa iko faint kabisa,haikulet ule wekundu unao kuruhusu ku connect,nmempelekea jamaa,baada ya kuset,akaniambia nimlipe buku 8.nlichoka kwa kweli,yaan kufanya tu settings ananiomba pesa yote hyo.naomba ufafanuz zaid kidogo.,maana hata dashboard siifahamu.samahan kwa usumbufu
 
ok tuanze taratibu

ukiona haileti huo wekundu na pale kwenye connect pamefifia mara nyingi huna setting ya internet, japo kikawaida uki install dashboard setting hukaa automatic, wakati mwengine hazikai hivyo utahitaji kuzitengeneza mwenyewe.

angalia hapa jinsi wanavyotengeneza
Unlock-Huawei-Zte.Blogspot.In: How to Set Profile in ETISALAT ZTE Modem Dashboard

kwa Tanzania
dial number ni *99#
apn ni internet mitandao yote
halotel ni b-internet.


turudi kwenye dashboard
mkuu dashboard ni hio software ya modem ambayo umetuma picha yake. tuchukulie mfano toka uinunue hio laptop umeshachomeka modem 5 tofauti tofauti na kila modem unaeka software yake, mwisho wa siku una software nyingi kwenye laptop yako hadi zinasababisha kuingiliana na kusababisha matatizo kama hayo.

hivyo hapo toa software za modem ambazo hutumii ibaki moja tu unayotumia kwa sasa.

kutoa driver
kila modem unayoichomeka inaeka drivers zake, hivyo wewe utatakiwa kwenda device manager kuzitoa,

click start kisha search device manager kisha iclick itafunguka

angalia hii picha


utakwenda kwenye modem halafu click zitatokea modem zote, kama zipo nyingi hilo ndio tatizo, utatakiwa uzitoe kwa ku right click kisha un install, kama ipo moja tu hio unayoitumia tatizo ni jengine.

ukizitoa utazima pc na kuwasha kisha connect upya modem na kuiacha ieke upya drivers.
 


Shukrani saana mkuu Chief-Mkwawa ..ubarikiwe saana kwa hii elimu uliyo nipatia.ntakuletea mrejesho soon
 
Uninstall modem dashboard ambazo hauzitumi, bakiza moja unayoitumia itakuwa ni muingiliano wa modem dashboard ndo maana inakuwa inaleta shida.
AU Weka new mobile partner kwa ku update dashboard kwenye modem.
 
Uninstall modem dashboard ambazo hauzitumi, bakiza moja unayoitumia itakuwa ni muingiliano wa modem dashboard ndo maana inakuwa inaleta shida.
AU Weka new mobile partner kwa ku update dashboard kwenye modem.
Shukrani kwa ushauri mkuu
 
Shukrani saana mkuu Chief-Mkwawa ushauri wako umenisaidia saaana.tatizo limeondoka kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…