mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Kilichotokea jana bungeni kwenye uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limeonesha kwamba vyama vya siasa vya upinzani vina viongozi wababaisha kuhusu demokrasia wanayodai haipo nchini.
Wakati CHADEMA inawasilisha majina 2 tu, na ya wanaume tu, yapitishwe bila kupingwa, CUF iliwasilisha majina ya CUF Maalim na CUF Lipumba.
Ni haohao viongozi wanataka tuwaamini kama watetezi wa demokrasia kwa kumkebehi, kumkashifu na kuchonganisha Rais Magufuli kwa wananchi waliomwamini na kumpa dhamana, kwa kura, kuongoza nchi hii.
Najiuliza, hivi hao viongozi wa upinzani wangepewa hiyo dhamana ya kuongoza nchi hii, wangeweza kweli kuunda safu ya kutatua matatizo sugu ya nchi hii, kama siyo kupata tiketi ya kuyafanya kuwa sugu zaidi!
Matatizo sugu ambayo Rais Magufuli, kwa utashi wake wa kisiasa (political will) na uthubutu wake binafsi anayashughulikia kuyatokomeza, kwa madaraka aliyo nayo Kikatiba, ni pamoja na:
1) Uozo uliotukuka Serikalini ikiwa ni pamoja na urasimu, uzembe, rushwa, ufujaji wa mali ya umma, na matumizi mabaya ya madaraka - silaha yake KUTUMBUA .
2) Kutamalaki kwa ufisadi - silaha yake ZIARA ZA KUSHITUKIZA
3) Vita dhidi ya buashara ya madawa ya kulevya - silaha yake KUWATAJA HADHARANI WAHUSIKA.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Rais Magufuli.
Na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani, hasa CHADEMA, mabingwa wa siasa za mitandaoni, vyombo vya habari, majukwaani na maandamano, tambueni UHARAKATI umepitwa na wakati. WAKATI UKUTA USIGOMBANE NAO.
Viongozi wa vyama vya siasa upinzani "Mfanye siasa kwa uhuru wa kujieleza Kikatiba. Ikosoeni Serikali kinaga ubaga, bila kuangalia aliyeko nyuma yenu, ilimradi mnafanya hivyo bila kuingiza uchochezi au maneno ya kashfa kwa viongozi wa Serikali" (Gazeti la Nipashe, Jumatani Aprili 5, 2017).