Mnyika: Serikali iache usiri miundombinu ya gesi!

Mnyika: Serikali iache usiri miundombinu ya gesi!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,308
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo John Mnyika, ameitaka Serikali kuweka wazi mradi wa miundombinu ya gesi asilia ambayo itahusisha ujenzi wa mitambo ya kusafishia gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na ujenzi wa bomba kuu la kusafirishia gesi hiyo kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini alisema hayo katika taarifa yake aliyoitoa jana Dar es Salaam kwa vyombo vya habari.

Alisema Serikali ilipaswa kuwasilisha bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika ili Bunge lishauri na kuisimamia Serikali kuanzia katika hatua za awali ili kuhakikisha maslahi ya Taifa yanalindwa na wananchi wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji huo mkubwa.

Mnyika alisema Julai 27, mwaka huu, alitoa pendekezo la Serikali kuweka wazi mradi huo, lakini haikuzingatia na badala yake Rais Jakaya Kikwete alifanya uzinduzi wa mradi huo Novemba 8, mwaka huu, huku akidai kuwapo usiri, jambo linalozua malalamiko katika maeneo ya mradi husika hususani Mtwara.

"Serikali irejee katika mapendekezo niliyotoa bungeni na itoe maelezo ya sababu za bomba hilo kujengwa kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam na ieleze kwa uwazi manufaa ya mradi huo na miradi mingine inayopaswa kutekelezwa katika mikoa ya Kusini kwa maendeleo ya wananchi husika," alisema Mnyika.

Alisema katika hotuba hiyo, pia alizungumzia ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi asili ya Mnazi Bay na SongoSongo kama sehemu ya mradi huo; ambapo Serikali inapaswa kueleza ni miradi ipi inayoambatana na mradi huo iliyopangwa kuwanufaisha wakazi wa Lindi na Mtwara ikiwemo kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 300 Mtwara na 230 wa Somanga Fungu (Kilwa).

Chanzo: HabariLeo
 
kwanini jamani selikali isijenge kituo cha kuzalisha umeme uko uko Mtwara na Lindi kuliko kutumia ghalama kubwa ya kuisafilisha gass mpaka dar es salaam..
 
JK anamiliki hii miradi,bandari+gesi+viwanda= Bagamoyo
 
ndio maana wenye gesi wametibuka na kuwa wakali kweli hawataki iende Bagamoyo eti m.Kwe.re. akileta mchezo atapelekwa The Hague
 
Ndio sababu leo hii wananchi wa Mtwara wameandamana kupinga kuporwa kwa maliasili yao!
 
najua itakuwa vigumu kusikilizwa as mtoa wazo anatoka upinzani.....hapa ndo ubaya wa siasa za nchi hii ukilinganisha na nchi zingine.....mada hata kama ni ya msingi inatazamwa kisiasa zaidi kuliko utaifa.....lakini usife moyo kwani hawatakuwa na njia ya mkato zaidi ya kuwaeleza watanzani mapendekezo yako....nasema haya kwa sababu muda huu wana mtwara wapo barabarani wakitaka kufahamishwa hiki ukipiganiacho....u will turn a hero bro....keep it up
 
hata kama tunasema mzee wa kaya kila kitu anadanganywa je hata hili la mikataba kuwa wazi nalo anadanganywa?hivi kama mkuu wa kaya hana maslahi yeyote kwani kuweka mikataba ya rasilimali zetu ikawa wazi atleast hata kwa wabunge tu nalo linahitaji marekebisho ya katiba?Jamani Mauritius kisiwa kidogo kinategemea uchumi kwa kulima miwa,uwekezaji biashara nje,uvuvi na utalii,lakini shule primary hadi high school bure,university 90% serikali inalipia,hospitali bure,usafiri wa mabasi mijini wanafunzi na wazee bure lakini nilipouliza siri ya mafanikio haya wakaniambia ni 1 tu;ni uwazi katika mikataba yote tena inawekwa gazetini.
sasa ndugu zangu hawa walioiba tangu baba wa taifa atutoke,mpaka leo hawaridhiki wakaiachia nchi hii ikapumua au mpaka machafuko wakose hata pa kuzilia hizo hela walizoiba ndo watajua kua wananchi wamechoka?
Tusibiri yana mwisho na yameshaanza kuonekana.
 
Back
Top Bottom