Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,966
- 51,111
Kabisa... Huyu Lissu alipigwa risasi zama za Magufuli ana kesi ya Uhaini zama za Samia. Sasa hapa tatizo ni watu au mfumo wa CCM ndiyo unaomtesa Lissu?Watajuana wenyewe...wamtoe Lissu huko Lupango.Mengine acha wamalizane wenyewe
Sad aiseeKabisa... Huyu Lissu alipigwa risasi zama za Magufuli ana kesi ya Uhaini zama za Samia. Sasa hapa tatizo ni watu au mfumo wa CCM ndiyo unaomtesa Lissu?
Ni heri Polepole anayesema ukweli hadharani hata kama ukweli huo umma unaujua kuliko mijitu mi-pumbavu na mi-binafsi na mi-nafiki ambayo inapiga zumari kwa watawala wa hovyo.Jee Polepole mambo anayoyasema ni ya kweli au ni uongo? Kama ni uongo ukweli ni upi na una ushahidi upi?
Wakati Polepole alipokuwa kiongozi wa CCM, aliyokuwa anayafanya yalikuwa na baraka za CCM au la. Kama yalikuwa ni mambo yake binafsi CCM waliwahi kumuonya?
Zama za Magufuli mambo maovu yakitendeka na Polepole akiwa kiongozi wa CCM, jee CCM yenyewe iliwahi kukaa kikao na kutoa tamko lolote au maelekezo kwa Serikali kukomesha yaliyokuwa yanatokea?
Leo Polepole anakikosoa chama chake na kwa sehemu usimamizi wa chama chake Kwa Serikali, jee asikilizwe na kuaminiwa au ahojiwe alikuwa wapi zama za Magufuli wakati maovu kama haya yakitokea?
Kama zama za Magufuli kulikuwa kuna uovu, na Sasa Kuna mfanano wa uovu ule ule, jee ni mambo ya Magufuli na Samia ama ndivyo CCM inavyotaka mambo yawe?
Maana kama Magufuli na Samia wote ni CCM na malalamiko dhidi Yao yanafanana, inawezekanaje kuitenga mbali CCM na uovu unaotokea badala yake tuwape watu wawili tu, yaani Magufuli na Samia?
Tatizo la Polepole ni kuusema ukweli ama ni yeye pia kutuhumiwa kuwa ni sehemu ya watenda maovu ila kwa Sasa watendao huo uovu si watu wa upande wake?
Polepole anastahili kupongezwa na kutiwa moyo. Amedhubutu kumvalisha paka kengere akiwa ndani ya chama.Kabisa... Huyu Lissu alipigwa risasi zama za Magufuli ana kesi ya Uhaini zama za Samia. Sasa hapa tatizo ni watu au mfumo wa CCM ndiyo unaomtesa Lissu?
Sawa tupe wewe ukweliSijui mtandao, sijui polepole, mara nani kapewa mgodi havisadiii kitu...
Polepole mzushi tuu,
twende na NRNE
Ukweli ni kwamba ni mfumo mbovu unaleta hayo matatizo yote, badala ya kupigania CCM , tupambane kubadilisha mfumoSawa tupe wewe ukweli
CCM ni majangili tupuUkweli ni kwamba ni mfumo mbovu unaleta hayo matatizo yote, badala ya kupigania CCM , tupambane kubadilisha mfumo
Polepole anapambania CCM,
(NRNE)
Hoja hapa ni mgodi wa makaa ya mawe. Tueleze ukweli wako nani sasa hivi anamiliki????Ukweli ni kwamba ni mfumo mbovu unaleta hayo matatizo yote, badala ya kupigania CCM , tupambane kubadilisha mfumo
Polepole anapambania CCM,
(NRNE)
Sawa, tueleze wewe mazito ili tulinganishe yako na ya Polepole.Mambo anayoyaongea ni mepesi ambayo tayari yalishaongelewa na vyama vingine vya upinzani na wanaharakati tena kwa kina zaidi,,kama itakua sio drama ya kuwapotezea watu muelekeo basi atakuwa anaisaidia CCM bila kujua...