Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,682
- 149,883
Homework hii si nyingine bali ni kukaa chini,kufikiri,kutafakari,kupima na kisha kufanya comparison katika utendaji kazi wa Mkuu wa Kaya hasa katika kile kinachoitwa kutumbua majipu.
Niliwahi sema hapa JF kuwa Mkuu wa Kaya ni mwepesi sana kuwachukulia hatua watumishi wa umma lakini ni mzito sana kuwachukulia hatua wanasiasa wenzake na nili-conclude hivi:
"Mkuu wa Kaya ni rafiki mzuri wa wanasiasa wenzake lakini ni rafiki wa mashaka sana kwa watumishi wa umma."
Kuthibitisha haya subirini kuona ni hatua gani zitachukuliwa kwa hawa:
1.Kampuni ya Lugumi na watuhumiwa wake.
2.Wabunge 18 wa CCM wanaotuhumiwa kwa rushwa na ambao tuliambiwa watashughulikiwa
3.Waziri Charles Kitwanga na kashifa hii ya Lugumi
Mnakumbuka tuhuma za mawaziri hawa na jinsi zilivyoisha kimyakimya?
1.Waziri mmoja kijana na dada yake kutajwa kumtapeli raia wa kigeni
2.Waziri alietuhumiwa kuvujisha siri kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo-kuvujisha siri ni kosa la kimaadili kwa kiongozi wa umma.
3.Yule waziri alietuhumiwa kuteua Mganda na kumpa uongozi katika Taasisi ya serikali.
4.Yule waziri mwingine alietajwa katika kashifa ya kuingiza mafuta nchini bila kufuata taratibu mwezi September mwaka jana wakati wa uongozi wa JK.
Hao wote mpaka leo hii wamefanywa nini?
Spidi ile ya kutimua watumishi wa umma mbona kwa hawa haionekani?
Kwa kifupi,spidi ya kuwajibisha wateule wake mwenyewe mbona haipo?