Mnaomchambua Augustine Okrah Magic kujiunga Yanga nendeni mkachambue mchele mpira umewashinda

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Augustine Okrah jana ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Yanga, sitaki kuwachosha saaaana ila huyu mwamba sio mtu wa kawaida, kama uliwahi kumuona marehemu Celestine Sikinde Mbunga basi utakubaliana na mm kuwa huyu mtu boli anajua.

Okrah kachezea Simba muda mfupi tu na watu tuliona shughuli yake, ilifikia wakati tukawa tunalalamika kwann anawekwa benchi, kuna shida gani, akiwa benchi akawa anapasha tu misuli mayai kibao yanakaangwa jukwaa la Simba, hivi nani anajua masaibu yaliyokuwa yanamkuta Okrah pale Simba, kwanini hamjiulizi pale Simba alikuwa majeruhi na iweje kule Ghana awe anacheza na amefunga c chini ya mabao 6 kwa muda mfupi tu tangu aondoke Simba, utasema mbovu huyo.

Okrah sio mlevi, hata sas hv Chama anatengenezeqa zengwe aonekane hana nidhamu, anatukana makocha ili mashabiki muamini kumbe sio kweli, Okrah Magic shughuli yake mtaiona huko Zanzibar, kama ni mlevi au hajui mpira subirini muone, msituchambulie mambo ya uongo hapa, kachambueni mchele huko.
 
Mchezaji mwenyewe ana miaka 30 yaani mjomba yake na Mzize lakini uto ni kama vile mmesajili 20's.
 
Mchezaji mwenyewe ana miaka 30 yaani mjomba yake na Mzize lakini uto ni kama vile mmesajili 20's.
Miaka ndio inacheza mpira? Current performance yake kwa sasa ikoje? Mbona mnae babu wa mababu ntibanzokiza na mnamuona Kama Messi wenu kwani Ana miaka mingapi? Wivu wa kike tu unawasumbua akuna lolote!
 
Mimi ni shabiki simba lia lia ila swala la kumuacha okrah na banda alafu ukaleta konde boi na onana nikaona wale viongozi ni wana utindio wa ubongo okrah magic alikuwa mtu wa ball anajua ball anajua aweke wapi mpira unaleta wazee akina saido unaacha okrah magic ukimuwek 10 pale kati pila linapigwa...

Ukimuweka 7/11 pira linaumizwa vibaya mno pale pembeni unamuacha banda unaleta kinene kifupi konde kaja kama nuksi simba na onana ubishooo mwingi hajui mpira uende wap kwa wakati gani......

Kibu ni sawa na kuobana simba hajui akili zake azitumie vipi kutengeneza nafac bala anataka sifa akiungana na rafik ake saido hawajui waisaidie simba katika kutengeneza nafac ball nguvu nyingi akili kisoda

All in all okrah magic mimi ni simba lakin nitabaki kusem wew ni mchezaji wa viwango vikubwa nidhamu yako nazani usingestahil kucheza africa ball ungekuwa huko duniani ukila mema ya ughaibuni
 
Back
Top Bottom