Mnaohama vyama kwa sababu ya watu fulani, gomvi ni itikadi na misimamo ya hovyo

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Hili niliseme tu kwa vyama vyote vya siasa nchini, kitendo cha mtu kuhama chama chake cha awali kwa sababu ya kumfuata kiongozi flani ni usaliti na kukosa misimamo thabiti ya itikadi alizo nazo mtu.

Kama umekua influenced na matendo au tabia za mtu flani kutoka chama flani na hujafukuzwa chama chako kwa maana ya kua mtu huru tatizo liko wapi? Kwani kubaki na itikadi za chama chako halafu ukamuunga mkono kiongozi flani hasa kwa mambo ya kitafa kuna tatizo gani?

Ni mfano wa wafuasi wa Mh Lowassa wakati anatoka CCM ambao walijua kua atakua rais wa Tanzania ili wao wanufaike, lakini baada ya kuukosa urais hawa watu walibaki kubabaika kwa sababu ya ufuasi wao na sio itikadi zao, ndio baadae waliamu tena kurudi CCM na huko wakapewa jina la "Ng'ombe waliokatwa mikia".

Hawa wanaohama Ku vyama vingine kwenda CCM kwa sababu eti JPM anafanya mambo makubwa ambayo wapinzani waliyahubiri miaka yote, lakini wajiulize JPM akiondoka madarakani akarithiwa na mtu kwenye siasa taofauti na zake na upinzani wakawa na gombea mwenye siasa madhubuti, je hawa wafuasi watarudi tena upinzani? Tuwaiteje hawa watu?
 
Wanafata haki huwezi kukaa nakiongozi unaona anapotosha umma halafu ukasimama jukwaani kumuunga mkono
 
Back
Top Bottom