MMU Imesababisha niibiwe

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,789
Reaction score
7,182
Wana JF,

Katika tukio lisilo la kawaida juzi nikiwa katika mgahawa mmoja pale sinza kwa remi, pale wanapopika vyakula vizuri Hot Food Hotel, niliishiwa kifurushi, nikatoka nje kununua nikiwa najaza vocha kwenye simu pembezoni mwa barabara, ghafla akaja bodaboda (Boxer) mimi sikuiona nilikuwa naendelea kuweka vocha nikakwapuliwa na jamaa wa kiarabu aliyekuwa amebebwa nyuma, nilijitahidi kuwarukia lakini nilishindwa kwani walirudi njia kuu kwenye magari yaliyokuwa yanaenda kasi, nilipopeleleza maeneo haya wanadai kuwa sinza siku hizi sio salama, nasikia waarabu/wapemba wanatokea msasani, wanapola na kuama maeneo,
WanaJF imenichukua muda sana kusahau kitendo hicho kwani kuibiwa live kunauma kuliko ile kuibiwa bila kujijua.
Nimewakosa sana, kwa sasa natumia ka Laptop.
 

pole, siku nyingine usikubali kuibiwa!
 
Pole mkuu.....yaan nmecheka kama mazuri vile.Kungekuwa na pikpik karibu ungewaungia tu
 
me nikajua umeibiwa mpendwa wako
 
hahahhaha miminjishanusurikaga kwenye UDA aisee duuh siku hiyo jion niko busy mmu kaja kibaka dirishani sasa kama mnavyojua uda ni mpya kwa hiyo hata vilock vya madirisha ni vipya

so kwa ubusy niliokua nao na simu nilivyoingia hata kukumbuka kufungua kioo sikufungua so kibaka anangangana kuvuta kiiooo nakuja kumuona kashangangana sana
nikamzomea oooooh dirisha lina kitasa
 
Nimechekaje ha ha ha yani hapo ulipomzomea kibaka umenimaliza
 

My god waarabu koko hao
 

Heheheheh kama nakuona unamzonea kibaka
 
Eti waarabu na wapemba hahahaha
Mbona uko zanzibar hatusikii kukwapua watu, mpaka wizi pia mnatusingizia? Salaaaaale
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…