Mke alirudi kutoka kazini na kumkuta mmewe ametulia sebuleni huku akiangalia TV. Mke, huku akiwa ameudhiwa huko kazini na nyumbani akakuta mmewe hamjali, alilalamika kama ifuatavyo:
Mke: Mimi sina anayenipenda...sina anayenijali.....yaani dunia nzima inanichukia mimi.
Mme (huku akiendelea kuangalia TV): Huo ni uongo mke wangu mpendwa. Una umaarufu gani mpaka huchukiwe na dunia nzima? Kwanza sidhani hata kama watu wa kabila lako wote wanakujua.