Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,544
Kuna jambo linanishangaza sana humu JF toka kwa baadhi ya watu waliokuwa wapinzani wakubwa wa UKAWA kwenye uchaguzi wa Mwaka 2015. Watu hao kwa namna moja ama nyingine wanaashiria kwamba UKAWA wana wajibu wa kutenda kitu fulani ili mambo ya kisiasa hapa nchini yaende vyema.
Kwanza wanawashutumu UKAWA kwa "kosa" lao hadi ajenda ya ufisadi "imekufa" kwa kitendo cha kumfanya Edward Lowassa kuwa Mgombea wao kwenye uchaguzi huo wa Mwaka 2015. Kwa maneno mengine CCM haina habari na Ufisadi ama yenyewe ndiyo fisadi hadi bila ya UKAWA kuusemea ufisadi hauwezi kusemwa na CCM. Hapa wanataka wale waliowakataa 2015 wawe wasemaji wao kuhusu Ufisadi. Swali la kujiuliza kabla ya mwaka 2015 jambo gani kuhusu Ufisadi ambalo lilisemwa na CUF, NCCR-Mageuzi ama CHADEMA likafanyiwa kazi ipasavyo na Serikali chini ya CCM?
Kila siku wanawashutumu UKAWA kwa kutokuwa na hoja zenye "maana" bungeni kama vile bunge zima limejaa wabunge wa UKAWA. Hata wasomi kama Harrison Mwakyembe wanabaki kulalama kwa nini UKAWA hawairudishi hoja ya Richmond Bungeni ili aweke "kila kitu" hadharani. Bungeni mambo yanaamuliwa kwa wingi, sasa kati ya UKAWA na CCM ni wabunge gani wapo wengi? Unatakaje bunge liwe imara kwa hoja madhubuti za wabunge toka UKAWA wakati kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 uliichagua CCM?
Kuna watu wanahoji Halmashauri zinazoendeshwa na UKAWA zimefanya nini tofauti na ilivyokuwa chini ya CCM. Kwa mfumo wetu ni kwamba Serikali za Mitaa zinaendeshwa na (Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania) Serikali Kuu. Unapochagua Rais wa CCM halafu unauliza mafanikio ya serikali za mitaa chini ya UKAWA, unajitia wazimu wewe mwenyewe!
Kila siku wanawatuhumu UKAWA kwa kutokuwa na shukrani kwa mambo yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na CCM. Lakini wenyewe hawataki kujiuliza shukrani inatokaje kwa mtu aliyeshinda uchaguzi na kupokwa ushindi wake mchana wa jua kali? Hivi siyo wao wanaotakiwa kuwa na shukrani kuishi na mtu uliyemdhulumu na bado badala ya kulipiza kisasi yeye anamwachia Mungu?