Habari za Nyerere day.
After six years of being in marriage naona kama ibilisi anakaribia kukata panga. I have two kids kwa huyu bidada but I see the end of road. Kila wakati nikiwaangalia hivi vitoto na wanapotaka kuelekea naona maji yanajaa katika macho yangu, wananipenda na nawapenda hasa lakini hatupendani na mama yao.
Nawaza sana niumie ili wabaki na furaha au niitafute furaha wao waumie? Mliopitia changamoto za divorcing hebu saidieni picha ya maisha after marriage.
Mkuu, mimi ni mtoto wa kulelewa na mama wa Kambo namshukuru mama yule ni mama mwema sana kwa upande wangu, yupo mdogo wangu wa kike ambaye naye tumelelewa pamoja lkn bahati mbaya sana hawakuiva na yule mama yetu aisee sitaki kurejea taswira za aliyopitia its bad na niliapa kuwa sitokuja kuwa sababu ya watoto wangu kulelewa na Mama wa Kambo.
Kwa kifupi nakushauri hivi;
1. Kuchokana kupo sana tu, lkn goes with certain period of time, vumilia ipo siku utaanza kumpenda tena mama yao, ndio sababu watu wanaweza achana leo wakarudiana baada ya miaka kadhaa kupita, that means wamerejea katika hali mpya ya kupendana hasa watoto wakiwa kiunganishi.
2. Kama huwezi ku balance mambo epuka michepuko maana u might fall totally kwa mchepuko nyumbani ukawa unaona ni kama jela/tanuri. (Kurogwa kupo)
3. Jitahidi kuwa sehemu tofauti na mama watoto wako mfano vacations na mitoko mingine can assist kwenye ku-reunite and revamping ur marriage.
4. Make sure maamuzi juu ya mahusiano yenu ni yenu yasiingiliwe na yyt iwe wa upande wako au wake, wengi hufurahia mabaya ya wengine yanapowakuta.
5. It might happen watoto wakawa wanalewewa na mama, certainly mama akaja kuolewa tena, wapo wababa wa kambo wenye kufanya unyama mkubwa kwa watoto waliowakuta kwa mwanamke including kuwalawiti etc....
Siafiki watoto kulelewa na mama wa kambo hutojua kinachoendelea kwa watoto ukiwa haupo, utajua ikiwa too late.
Testimonial
Ninaye shemeji yangu (dada wa mke wangu) ameachana na mumewe, katika vitu huwa anatusihi ni kufikia hatua aliyofikia yeye maana inamtesa kuona wale watoto wanavyohangaika na kuteseka kwa sababu ya wao kuachana. Mm nimechukua jukumu la kumlelea mwanae mmoja kwasababu ya mateso aliyokuwa akipitia huyo mtoto.
Nikutakie kila la kheri na busara kwenye uamuzi wa hili. Kumbuka kosa pekee gumu kusameheka ni uasharati mengine yanarekebishika na kusameheka.