Sijui unamananisha nini unaposema mlinzi wa Rais. Kama unamananisha yule Ofisa wa jeshi mwenye sare ambaye unamananisha siku zote huwa nyuma ya Rais basi yule siyo mlinzi.
Yule ni ADC ambaye shughuli yake ni kuwa karibu na Rais kwa mambo mbalimbali ya kijamii na kazi kwa Rais.
ADC anaweza kuwa kazi yake ni kubeba speech kwa Rais, kumsaidia kwa mambo mengine kama kuangalia kiti kimekaaje na kadhalika na kadhalika.
Kwa upande mwingine ADC ni symbolic gesture ya madaraka ya Rais. Na ukumbuke sio marais wote wana Ma-ADC. Ukichunguza kwa makini utaona si rais kumuona ADC kwa Rais wa Marekani.
Kwa upande wa walinzi wa kiukweli ni kuwa wao hawavai sare. Walinzi hao wako wengi ingawa ni kweli yuko mmoja au wawili ambao siku zote ndiye yuko karibu na Rais. Mlinzi huyo aliye karibu na Rais hawezi kuchaguliwa na Rais.
Kikosi cha ulinzi cha Rais ndicho kinamteua mlinzi huyo kutokana na vigezo mbalimbali of course vikiwemo vya ukakamavu, ujuzi wa mafunzo ya mapambano kama karate, loyalty kwa system na kwa rais, muonekane wake na kadhalika na kadhalika.
Sidhani kama Rais anaweza kuwa na mkono katika uteuzi wake ingawa inawezekana pengine baada ya muda Rais anaweza akasema kuwa abadilishiwe mlinzi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za majungu na kadhalika.
ADC huteuliwa na Jeshi lakini inawezekana pengine Rais akawa na 'ushawishi' katika uteuzi wake. Hapa neno 'ushawishi' liko kwenye mabano kwa makusudi.
Inamananisha vikundi mbalimbali katika jamii ambavyo viko karibu na Rais vinaweza vikapenyeza jina la ADC. Lakini kwa nchi zinazozingatia mfumo mzuri wa utendaji wa kazi na kuacha pembeni masuala ya ubabaishaji si rahisi kwa ADC kuteuliwa kiushikaji.Kuhusu hali ikoje kwa Tanzania mimi sijui. Tafuteni wenyewe uteuzi unakuwaje.
Duh! hii nayo elimu nzuri. Watakuja wajuzi wa mambo haya aatujuze. Tena ngoja nii'subscribe topic hii.
Nijuavyo mimi(na naamini ni sahihi,watakuja kunikosoa wajuzi zaid), nikwamba, MLINZI huyo huchaguliwa na Rais kwani anapaswa kuwa anayejuana naye au mtu wa karibu sana mfano shemeji, mdogowake, ukoo wake na mengine kama hayo.
Nimeyasema hayo nikirejea hisia zangu kwamba, ni lazima nimchukue mtu ambaye ana'fall ktk categories hizo for my benefits.
Kwa upande mwingine, unaweza ukakuta mtu huyu anachaguliwa na system kwa maana ya Jopo au Kikosi cha ulinzi wa Rais.
Ni hayo tu.
yule jamaa sio mmoja , huwa wapo zaidi ya mmoja , na yule sio bodyguard bali ni mpambe tu.. jaribu kuangalia picha tofauti za mheshimiwa raisi , utaona kwamba yule jamaa huwa anakuwa tofauti
Mimi wanaojiita wazee wa jf! na wanadai wakati huo walijadili mambo ya maana naomba wanijibu maswali yangu.
1, kwanza waniletee hizo link za maana ambazo zilipositiwa mwaka 2006 hadi 2011.
2, majadiliano yao mazuri yalisaidia nini? bona wao wezi wamaescrow walichanguliwa 2005 na 2010.
3, katika uchumi mbona nchi yetu ni masikini tu, pamoja na majadiliano yao mazuri?.
mpambe wa rais ni mmoja tu,aliyekuwepo awali alipandishwa cheo kuwa brigedia gen hivyo amerudi jeshini........wanaobadilika ni walinzi maana ni kundi la watu wengi kdg
Haiwezekani akawa mmoja. Inamaana yeye haumwi? Hana dharura? Au akiwa na dharura ndio raisi siku hiyo atakuwa hana mpambe? Raisi ndio mmoja , ila wengine wote wanabadilika.. Nitajitahidi kukuletea picha
Aisee........mi huwa najua ni yule yule..........na mbona huwa wanafanana.......?......kuna maumbo maalum........?