Mlengwa wa mlipuko alikuwa balozi wa Vatican?

Mlengwa wa mlipuko alikuwa balozi wa Vatican?

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
24,859
Reaction score
56,851
Ndugu WanaJamvi;

Kwa muda sasa kumekuwa na hoja mbali mbali juu ya uhalali wa uwepo wa Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania. Katika hili kuna, kuna pande kuu mbili zinazokinzana - wanaopinga na wanaounga mkono kama ifuatavyo:-

(1) Wanaopinga: wanajenga hoja kwamba kwa kuwa Vatican ni nchi ya kidini (Kikatoliki) na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba, Tanzania haina dini hivyo sio sahihi kwa "nchi" hiyo kuwa na ubalozi wake hapa nchini. Wengine wanaenda mbali zaidi kiasi kwamba hawataki kukubali Vatican ni nchi. Hata hivyo "wanalegeza" masharti kwamba kama Vatican ina ubalozi wake hapa basi ni halali kwa Tanzania kama nchi kuwa mwanachama wa taasisi za kidini kama OIC. La kushangaza hapa ni kwamba kwao uhalali wa Ubalozi wa Vatican utakuwepo endapo Tanzania itakuwa mwanachama wa hizo taasisi za kidini vinginevyo sio halali.

(2) Wanaounga mkono:hawa wanajenga hoja kwamba; kwanza Vatican ni nchi huru, yenye mamlaka kamili, na inayojitegemea kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya neno "nchi" lilivyo na linavyotambulika kimataifa. Na wanaenda mbali zaidi kwamba sio tu kwamba Vatican ni nchi bali inatambulika hivyo rasmi na UN. Hivyo, kwa hoja hii, ni sahihi kabisa Vatican na Tanzania kuwa na mabalozi wanowakilisha nchi zao.

MLIPUKO WA LEO:

Kati ya viongozi wakuu wa Kanisa waliokuwepo kwenye shughuli ya leo kule Olasiti, Arusha, ni Balozi wa Vatican nchini Tanzania ambaye pia ana hadhi ya Askofu Mkuu. Hivyo zimeanza kuzagaa habari pengine kutokana na ukinzani wa baadhi ya makundi kutotaka Vatican kuwa na ubalozi wake hapa nchini, kuna uwezekano pia mlengwa mkuu alikuwa Balozi husika. Mimi sijui, ila kama GT tudadavue na hili.

LAWAMA:

Lawama pia zimeanza kuelekezwa kwa serikali kwa kutochukua hatua madhubuti na kwa wakati pindi zinapotokea chochoko kama hizi katika jamii. Kwa mfano, hili la upotoshoji wa uhalali wa Ubalozi wa Vatican hapa nchini propaganda zake zimeenezwa kwa muda mrefu sana kwa njia mbalimbali kama mihadhara, ibada, na hata kwenye media mbalimbali. Badala ya serikali kutolea ufafanuzi wa uhalali wa huo ubalozi, imekuwa kimya bila kujali athari za baadaye za propaganda hizi chafu pengine kwa falsafa ya "ni upepo tu utapita". Je, ni kweli serikali inastahili lawama katika hili?

HITIMISHO:

Je, kama serikali ikitekeleza madai YOTE ya haya makundi, kuna uwezekano wa chokochoko hizi kukoma na hivyo nchi yetu kuwa ya amani na utulivu kama ilivyoachwa na waasisi wetu? Lakini je, walengwa wa haya matukio ni wakatoliki peke yao? Au ni pamoja na makundi mengine? Haya matukio yana uhusiano wowote na siasa za nchi yetu? Mimi sijui, nalileta kwenu wakuu.
 
Mbona Iran nayenyewe nchi yakidin awasemi?
 
  • Thanks
Reactions: PSM
Mkuu mleta mada nchi yetu kwa sasa hali ilivyo ni kuomba tu Mungu,maana wenye dhamana wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini hawasikii.
 
Mbona Iran nayenyewe nchi yakidin awasemi?

Sio tu Iran kuna Saudi Arabia, Oman etc. Je itakuwa sahihi Wakatoliki nao wakianza kuwalipua kwa mabomu mabalozi wa nchi za kiislamu?

Tukubali tusikubali there is something wrong in islamic teaching. Islam teachs more HATE than LOVE, while Christiniaty teachs LOVE. That is the difference between CHRISTIANITY and ISLAM.
 
sasa ni mwaka wa 8 nchi hii haina raisi wala kiongozi wa nchi tunaishi kwa neema ya mungu tu
 
Sasa kutoka vita ya Kuchinja tunaelekea vita ya kugombea Balozi za nje?? Hizi ni Dalili za Laana kuu kwa Watanzania! Watanzania wa 1960 walikuwa na upeo mkubwa kuliko wa 2013!
 
MaCCM yanalea na kuchochea uchochezi wa kidini kwa maslahi ya kisiasa.
 
KAMA KUNA MTU BADO ANAKUMBUKA OMAR MAHITA NA 'TOROLI YA VISU VYENYE TOMATO SAUCE', KILE KINACHOITWA 'UGAIDI' JIJINI ARUSHA UNA MALENGO YA KISIASA KUGAWA JIJI HILO KIDINI KUNAKOELEKEA UCHAGUZI WA MADIWA. WaTanzania wala tusipumbazwe kama mazezeta hivi; hakuna cha(1) Sheikh Ilunga, (2) Al-Shabaab, (3) Al-Qaeda wala nani anayewadhuru wananchi kwa malengo ya kuleta hofu na hali ya kutokuaminiana kati ya Wakristo kwa Waislamu nchini. Kwa kufuatilia matukio ya 'Ugaidi wa Kuchonga' na matukio ya hivi karibuni jijini Arusha lazima ujiulize kwamba kati ya watajwa watatu hapo juu na (4) Serikali ya CCM, ni yupi kati ya wote mwenye kuweza KUNUFAIKA kisiasa na ulipuaji ovyo wa mabomu A-Tauni??????? Na kwa mtindo huo ndio maana kati ya michango yote juu ya tukio hili la kusikitisha sana, hakika nimeweza kumtambua mwenzetu huyu, Mkuu Lyamunda, kuwa kweli ni great thinker mwenye uwezo mkubwa kuona ujumbe ilioko nyuma ya ujumbe unaoonekana wazi kwa kila mtu. Ni masikitiko yalioje kuona jinsi gani serikali ya CCM inavyotumia dhana ya 'Ugaidi' kwa maslahi kisiasa kwa mtindo ambao sio kabisa. Wakristo kwa Waislamu kote nchini, tafadhalini kaeni mbali sana na hizi mbinu chafu za CCM na serikali yake kutumia hizi mbinu za ki-Nazi kutafuta kutugawa kwa misingi ya kidini kwa kutumia silaha yao mpya ya 'Ugaidi unaosimamiwa na vijana wake'. 'Gaidi wetu wa kuchonga' yuko ndani ya serikali hata kesho. Tena mbinu hizi zikiendelea zaidi basi huenda tukalizimika kutaja kwa majina baadhi ya vijana wa serikali ya CCM walipata kutumwaa Zanzibar miaka ya Mahita dhidi ya CUF kwa matukio kama haya haya.
Tokea mlipuko wa Arusha ulipotokea, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana habari hii, nimepelkea kuamini kuwa kwa sasa kuna dini mpya mbili amabazo ni hatari sana CHADEMA NA CCM!! haswa humu katika JF. anyway yana mwisho haya lkn kumbukeni kuwa tunaiuza nchi kwa bei rahisi sana!! Angalau nimefarijika kidogo kukutana na hii!! source ikiwa ni ZITO kabwe! #Nyufa........ Maadui hupita kwenye nyufa. #CUF ilipoitwa chama cha Waislam, hata watu wenye heshima nchini waliamini. Nyufa...... #CHADEMA ilipoitwa chama cha wakristo hata watu wenye akili wakaamini. Nyufa..... #Udini upo, #Udini haupo ni kauli za kupanua nyufa. Kama Taifa tuzibe nyufa hizi. Tukae tukiri makosa, tukatae kugawanywa. Maadui wanatumia nyufa hizi kuingia kubomoa Taifa hili. Tusome alama ukutani. Epuka kauli za chuki. Hate speeches must be made illegal. There is so much hate in our society now, in communities, within communities, against communities. We are a Nation- United Republic of Tanzania na kama huamini uhatari wa dini hizo mpya, basi endelea kufuatilia response ya wanajumuia hapa!! watu wanaabudu vyama kuliko UKWELI? yaani bila kujua wanauza kwa bei rahisi sana iwe kwa kauli au matendo yao, adui mkubwa hawamjui... Mola atuepushe na balaa...
 
jamani mie naomba mwenye picha anitumie za majeruhi ili tuzione na tujue kiwango halisi cha maumivu haya ili tuombeane,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom