Mlegezo

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,205
4,405
MLEGEZO
.




1)wengi japo wanasema,kama umekata gogo.
Mabwe pande mji mwema,uliopewa kisogo.
Tambua jua mapema,hilo jambo ni kipigo.
Mlege wazua tata,utata wenye mashaka.




2)wengine jali wanena,vazi hilo gerezani
Lilianzia na jina,mlegezo taabani.
Wavaaji mtanuna,kwanilo maana gani.
Mlege wazua tata,utata wenye mashaka.




3)mkanda umekatika,ama nguo hikutoshi.
Yaonwa kama yashuka,hilo haliba ubishi.
Kalamu iliandika,tena ile waandishi.
Mlege wazua tata,utata wenye mashaka.





4)ama yote matangazo,wayashusha hadharani.
Ila hilo angalizo,watangaza suti ndani.
Basi washa na chetezo,kwa mtumba wa sokoni.
Mlege wazua tata,utata wenye mashaka.




5)vipi moshi ukitoka,kilichosagwa chakula.
Wahisi hakitanuka,kile ulokwisha kula.
Wavaaji wanacheka,kama washikaji dola.
Mlege wazua tata,utata wenye mashaka.
6)alaa kumbe ni mbege,jamani sikutambua.
Acha lidondoke zege,beleshi ije kuzoa.
Hata wakiwahi ndege,nyumba waende jengea.
Mlege wazua tata ,utata wenye mashaka



Shairi:MLEGEZO.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382486.
 
Back
Top Bottom