Zanzibar imekwama tokea Jecha kufuta uchaguzi wa 2015. Hali ya Zanzibar ni mbaya .Yaliyotokea kwenye uchaguzi leo si pahala pake lakini haya yanayoendelea.
Kwanza ikumbukwe kuwa hakuna tena GNU ila kuna utawala wa chama kimoja. Jamii imeparaganyika na kususiana.
Uchumi umekuwa mgumu kwa watu wa kipato cha chini. Serikali imezuiwa misaada na mashirikiano na baadhi ya mataifa hali inayoathiri upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi. Umoja na mshikamano umepotea kiasi cha hata viongozi wa dini hasa kisiwani Pemba kutoipa ushirikiano serikali kwa masharti ya kutaka haki itendeke ili kuondowa dhulma ya uchaguzi.
Viongozi waliopo madarakani badala ya kuhubiri huo umoja nao wanahubiri visasi na kukuza mgogoro zaidi. Baraza la wawakilishi kama muhimili linaleta mihemko ya kisiasa kwa kuitaka serikali iwashughulike wapinzani kwa kupitisha maazimio. Hali hii inazidisha mtafaruku badala ya kutatua. Haya yalitokea hapo juzi kwa kuitaka serikali ichukuwe hatua madhubuti ikiwemo kukamatwa kiongozi wa CUf Maalim Seif.
Kwa Upande wa uongozi wa Jamuhuri ya Muungano ni kama wamejitenga na kinachoendelea Zanzibar. Huoni jitihada tokea mkwamo wa uchaguzi wapo kimya huoni njia za kutaka kutatua mgogoro. Taasisi za kijamii ziko kimya, Asasi za kisheria ziko kimya, wanasiasa wako kimya. Hali inazidi kuwa mbaya. Tunaona mazingira ya vitisho zaidi kutoka pande zinazovutana. Mafahali wanapambana nyasi (Raia) zinaumia.
Hakuna mwelekeo wala njia za utatuzi zilizo wazi. Ni kutishana na kutunushiana misuli.
Wako wapi watetezi wa wazanzibari? Mkwamo huu unawatesa wanyonge na kuiviza Zanzibar kimaendeleo, kijamii kiuchumi na kisiasa
Nini hatima ya Zanzibar?