Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ni mfano wa kuigwa!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,664
Habari wana JF

Mh.Paul Makonda akizungumza na Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi anasema tarehe 5/1/2016 ujenzi wa shule 7 katika wilaya ya kinondoni ulianza na amezindua kampeni ya kuchangia ujenzi wa shule Saba za kata katika wilaya ya Kinondoni ili kupunguza upungufu wa shule katika wilaya hio ambapo zitachukua zaidi ya vijana 3183

Akiongelea maendeleo ya Kampeni hio amesema inaenda vizuri na michango inaendelea kumfikia na witikio umekuwa mkubwa sana!

Akitoa tathimini fupi amesema amepokea Mifuko 500 ya cement toka kwa Dr mwaka....mifuko 1000 ya cement toka kwa watu mbalimbali na umoja wa mafundi geleji wametoa mifuko 50 ya cement! Amesema ameamua kujenga shule hizo saba kuondokana na tatizo la upungufu wa shule katika wilaya ya kinondoni na kuongeza kuwa Elimu ni njia bora na pekee ya kuwapa urithi wadogo zetu na watoto zetu! Ameendelea kuwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kuchangia kwani Kutoa ni moyo na si utajiri ameomba mwenye chochote hata mfuko mmoja wa simenti iwe hata tofari moja au mawe na mchanga wanapokea chochote

MAONI YANGU!

Mh.Paul Makonda ni mfano wa kuigwa kwa wakuu wa mikoa na wilaya zote hapa nchini katika utendaji wa kazi,Hata wabunge pia ni lazima wajifunze toka kwa Makonda na si kubaki kuilalamikia serikali inafanya nini ni wakati wa wao pia kusema serikali wameifanyia nini

Ukiacha maneno yanayo semwa kuhusu Mh.Paul Makonda utendaji wake wa kazi wananchi wengu wameupenda pamoja na mapungufu machache alio nayo
 
Bozongwa hilo hamna kitu Zaidi ya kufanya kazi kwenye media kama ilivyo serikali ya awamu ya tano.
 
Attachments

  • 1452874907744.jpg
    1452874907744.jpg
    56.1 KB · Views: 66
Kauli mbiu yake anakwambia Usipige maneno piga kazi afanye kwenye media au wapi kikubwa tunaona anayo yafanya
CCM ndiyo mabingwa wa kauli mbiu maendeleo ni vitendo. Miaka inapita na kauli mbiu ni hasara tu.
 
Anajitahidi, lakini tunatakiwa tuangalia hizo donation zinatoka kwa nani kwani wengine wanatumia kutoa msaada kama njia ya kujisafisha kwenye jamii.
 
Tunampongeza ila hapendeki. Na hata akifanya mazuri namna gani atawin watu wachache sana wenye kumpenda. Na hakuna kitu kinamtesa binadamu kama kutokupendeka hasa unapojitahidi kujipendekeza.
 
Habari wana JF

Mh.Paul Makonda akizungumza na Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi anasema tarehe 5/1/2016 ujenzi wa shule 7 katika wilaya ya kinondoni ulianza na amezindua kampeni ya kuchangia ujenzi wa shule Saba za kata katika wilaya ya Kinondoni ili kupunguza upungufu wa shule katika wilaya hio ambapo zitachukua zaidi ya vijana 3183

Akiongelea maendeleo ya Kampeni hio amesema inaenda vizuri na michango inaendelea kumfikia na witikio umekuwa mkubwa sana!

Akitoa tathimini fupi amesema amepokea Mifuko 500 ya cement toka kwa Dr mwaka....mifuko 1000 ya cement toka kwa watu mbalimbali na umoja wa mafundi geleji wametoa mifuko 50 ya cement! Amesema ameamua kujenga shule hizo saba kuondokana na tatizo la upungufu wa shule katika wilaya ya kinondoni na kuongeza kuwa Elimu ni njia bora na pekee ya kuwapa urithi wadogo zetu na watoto zetu! Ameendelea kuwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kuchangia kwani Kutoa ni moyo na si utajiri ameomba mwenye chochote hata mfuko mmoja wa simenti iwe hata tofari moja au mawe na mchanga wanapokea chochote

MAONI YANGU!

Mh.Paul Makonda ni mfano wa kuigwa kwa wakuu wa mikoa na wilaya zote hapa nchini katika utendaji wa kazi,Hata wabunge pia ni lazima wajifunze toka kwa Makonda na si kubaki kuilalamikia serikali inafanya nini ni wakati wa wao pia kusema serikali wameifanyia nini

Ukiacha maneno yanayo semwa kuhusu Mh.Paul Makonda utendaji wake wa kazi wananchi wengu wameupenda pamoja na mapungufu machache alio nayo
Anajenga shule au anajenga majengo? Kujenga shule na kujenga jengo ni vitu viwili tofauti. Mimi nataka serikali yenye viongozi wanaofanya kazi kwa weledi na kufuata taratibu na sheria. Hii habari na kila kiongozi kuamka na kufanya anachojisikia ni uongozi ulioshindwa na usio na vision. Vitu hivi vitasababisha nchi isiwe na mipango endelevu na kila mtu aishi kwa kupanga na kufanya anavyotaka. Tutajikuta tuna majengo yasiyokidhi viwango na yasiyopangiliwa. Nadhani huyu jamaa anatafuta sifa zisizo na maana
 
haya makampuni ambayo yanajitolea chochote huenda yanawalakini!, kibiashara!/ au ndio Yale yaliyokuwa yakifaidika katika utawala uliopita
 
Dr. Week Year tena .naipenda hii serikali..bifu la Kigwa na huyu Dr. Nimeanza kulijua.
 
Back
Top Bottom