Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob leo Ijumaa 22/4/2016 amemtambulisha rasmi Mkuu Wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Salum Hapi mbele ya waheshimiwa Madiwani wakati wa Kikao cha Baraza Maalum la Madiwani.
Akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Boniface amesema anamshukuru Rais kwa kumteua kijana mwenzake ambae ni mchapa kazi, na kuahidi kumpa ushirikiano, akikuta kazi iliyoachwa na mkuu wa Wilaya aliyepita aliifanya kwa asilimia 60 yeye aongeze afikishe asilimia zaidi yake.
Kinondoni inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za ufisadi uliokithiri, rushwa, taka, migogoro ya ardhi, huduma za afya, elimu n.k. Meya amemuahidi Mkuu hiyo wa Wilaya kumpa ushirikiano, akiongea Mstahiki Meya amesema " Ingawa wewe Mkuu Wa Wilaya upo reli ya kati Na mimi nipo reli ya TAZARA lakini naahidi kukupa ushirikiano, mimi namjua Mhe. Salum toka tukiwa Chuo Kikuu yeye akisoma Sheria Na mimi nikisoma ualimu, kwa nafuraha sana kuwa nae pamoja kuhakikisha tunaondoa kero zinazoikabili Manispaa ya Kinondoni na kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali itikadi".
Kikao hicho ambacho alikaribishwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Hapo, kilikuwa ni maalum kwa ajili ya marekebisho ya bajeti ya Manispaa ya Kinondoni na kufanikiwa kuokoa Bilioni 1.7 ambazo zilikuwa zitumike kwa ajili ya overtime na posho.
Pesa hiyo imeelekezwa kwenye kununua madawati na mambo mengine, kutekeleza agizo la Rais Magufuli ambalo alilisema juzi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa Ujenzi wa fly overs eneo la TAZARA jijini Dar es salaam.
"Kinondoni imeshakuwa na wakuu wa Wilaya 17 katika vipindi tofauti tofauti, kila mmoja ana vipaumbele vyake, nakuta Mhe. Mkuu Wa Wilaya ya Kinondoni uwe na goals zako, tutakupa ushirikiano, ili ufikie malengo, inaonyesha Kiongozi wengi waliopita Kinondoni baadae wamekuwa Kiongozi wakubwa, nataka nikupe na wewe unaenda juu zaidi, usiishie ukuu wa Wilaya" amesema Mhe. Boniface
Akiongea Mkuu Wa Wilaya ya Kinondoni mbele ya Baraza la Madiwani Mhe. Salum Hapi amemshukuru Meya kwa kumkaribisha kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani na kumtambulisha rasmi, alitamani sana yeye ndo awe wa kwanza kufika ofisini kwake lakini yeye alimuwahi akaenda ofisini kwake na leo kumualika kwa ajili ya kumtambulisha.
Akieleza vipaumbele vyake Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni amesema kwanza kabisa hajaridhika kama Kinondoni kuna watumishi hewa 34 tu, hivyo ameagiza uhakiki upya, Kinondoni ni Wilaya ambayo inaongoza kwa changamoto nyingi zikiwemo za ufisadi, migogoro ya ardhi, taka, wanafunzi kukosa madawati. Amemshukuru Meya wa Kinondoni kwa kumuamini pia yeye anajua Meya wa Kinondoni ni Kiongozi makini na anao uwezo mkubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili Manispaa ya Kinondoni, wakiunganisha uwezo wao na uzoefu wataweza kufikia malengo.
Kinondoni kuna uozo mkubwa, watu wameliibia taifa sana, sasa imefika mwisho, na walioiba wakibainika wafikishwe mbele ya Sheria na ikiwezekana kurudisha pesa walizoiibia nchi.
Mkuu Wa Wilaya amesisitiza katika kuiongiza Kinondoni isimamiwe haki na uadilifu akija mtu na dili au kutoa rushwa akataliwe.
Akiongea Mbunge wa Ubungo Mhe. Saed Kubenea amesisitiza nchi iongozwe kwa Sheria,taratibu na kanuni, sio mtu kujiamulia mambo huku anajua anavunja Sheria na taratibu za nchi. "Hii ni nchi ina Katiba,sheria, taratibu na kanuni lazima ziheshimiwe ili tuweze kufika tunapopataka,tupambane na ufisadi na rushwa katika nchi yetu, vigogo wengi wakubwa katika nchi hii wamehusika katika ufisadi lakini kuna kulindana ifike mwisho" amesema Mhe. Kubenea