Mkuu wa nchi HANA maadui nyumbani

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Nitengue na Kubadili jumla fikra hizi ambazo wakuu wa nchi wanazo juu ya wananchi wao kuwaza kwamba kati ya raia wake wamo maadui zake..

fikra hii ni ya kinyonge, na fikra dhaifu sana, na fikra inayodidimisha utashi wa wakuu wa nchi wengi. kujenga na kuhifadhi nadharia kichwani kwamba kati ya raia zake, ana wa chama hiki cha kisiasa au kile, ama mtu mmoja mmoja sehemu flani ambaye ni raia wa nchi yake anaweza kuwa adui yake, ni makosa makubwa mno.

Kila raia, kwa nafasi yake na sehemu yake, ana mapenzi makuu sana na uazalendo usio pimika na nchi yake. kila raia (isipokuwa mgeni) ndani ya taifa lake anao ndugu zake wengi tu, marafiki na wapenzi, wazazi na watu wanao mzunguka, hakuna wala haipo dhanio kwamba raia huyu anaweza kuisukumizia nchi yake "mtaroni" ipotee. nchi ikipotea ni wazi na yeye kapotea. hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye yuko tayari kujipoteza.

lakini nchi kama familia ina watoto wa namna na namna, kuna wale ambao wanaharaka sana tufikie pahala wanapoamini inawezekana hawa huwa wana changamoto yao, kuna wale ambao kazi yao ni kuchungulia makosa na kuyakosoa kwa sauti kubwa nao wana changamoto yao, kuna wale ambao tu hawaridhiki, hata wapewe nini wao watapiga kelele tu nao wana changamoto yao, kuna wale ambao ni mizigo, ambao mara zote wanaunga mkono kila kitu, wako kama maroboti, ukicheka nao wanacheka, ukilia nao wanalia, na sikuzote ni NDIO MZEE!!.. ni mizigo, ukifanya maamuzi yenye makosa wao wanakushangilia na kukutetea kwa nguvu na kuyabatiza maamuzi hayo kwa kila tamshi lilirorembwa, na kesho ukiyatengua maamuzi hayo hayo..hao hao watajipindua kama vinyonga na kukuunga mkono wakiyaponda maamuzi ambayo jana waliyabatiza majina matam matam, hawa ni mizigo lakini wote ni wana familia..

Ukikusanya familia hii yote kwa makundi yao kama mkuu wa nchi, lazima uwe na jicho la kupenya mbali zaidi na kugundua kila mmoja kwa nafasi yake nia yake ni njema juu ya nchi yake. unapo kuwa kiongozi na pia ukweli kwamba wewe ni binaadam, ni kweli yapo maneno yanauma ukiyasikia, kama yanakuvunja moyo, kama yanakukebehi, ukiwa na kamoyo kadogokadogoo ni rahisi kukasirika na kuwaza kupoteza watu, lakini ukiwa na moyo ulio jaa unachungulia ndani ya hayo maneno makali unapata majawabu ya vitu vingi sana. kuna watu wana maneno machungu lakini matamshi yao ndiyo yanayo endesha nchi kama ukiyazingatia.

Asante.

N.B niweke nyongeza tu ambayo sio muendelezo wa hapo juu kwamba, Mtawala unapo jitabaisha kwamba wewe ni mtu wa haki, usawa, kazi na nidhamu .. na ukiweka mkono wako kutekeleza hayo kwa nguvu zote, ukajizolea mashabiki ndani na nje ya nchi, jua wazi hapana msimamo usio na mitihani, unafukuza yule!1, unatumbua huyu !!, unatimua yule!, Wananchi wanakushangilia, ili Mola aendelee kukujazia nguvu, anakuletea Mtihani, mtu wako unaye mpenda tena unaye mtuma kutumbua wengine na yeye kumbe ana vigezo vyote vya kutumbuliwa..!! hapo mwenyezi Mungu anakutega!! je utaendelea kuwa mtu wa Haki au utautia doa utawala wako Jumla.. na Utawala ukisha tiwa Doa ndio mwanzo wa kudorora na kuporomoka kwa kasi.

"brain za nchi tunachorachora tu.."
 
kazi ya kuongoza nchi ni kazi shirikishi
 
Ukiona kiongozi kazi kubwa ni kufanya kampeni ili baada ya kampeni aanze mapumziko ndio wenye ufikiri huu.....!!!! Marais wa aina hii ni watu walioshtukizwa kuwa marais yaani hawana utashi wa uongozi hata kidogo!! Rais analazimisha anayoyaamini nje ya katiba ya nchi tushirikiane naya ni kututaka tumruhusu awe juu ya katiba na kumiliki haki zetu zote, katiba inatutaka tushirikiane na Rais kutawala nchi kwa mujibu wa katiba ndipo ushirikiano wetu ulipo, hatuwezi kushirikiana na Rais

Mfano :

kwa jinsi alivyopata vitanda vya muhimbili kwa mbinu za mchangani na siyo kwa taratibu zilizopo ambazo uwepo
wa taratibu hizo unapunguza urasimu, upendeleo, rushwa na ubadhilifu wa mali za uma. Rais akaruhusu utaratibu batili ili aonekna kaweza ... utaratibu ule ukiendelea hakuna vitanda kutoka MSD vitaenda mikoani tena.

Rais anafurahishwa na ulazima wa kuliangamiza moja ya makabila ya nchi yake mwenyewe halafu eti liwe ni jambo shirikishi? Huku si kuhuisha uadui ili nchi istawalike baada ya yeye?

Rais anayetaka kumaskinisha watu wake wenyewe kwa kutafuta uhalali wa ukabila wake dhidi ya Kabila asilolitaka anawezaje akawa mahiri wa kuwatajirisha hao anaowapenda na kuwakubli?

Rais anayeamini utawala wa taifa lolote hutegemea nguzo 1 na siyo 3, kwamba mwenye mamlaka na amri ndio kiongozi wa nchi, wengine wote wakimbizi wanaopewa hifadhi ktk nyumba ya Rais ...!

Rais asiyeamini wananchi wake, haamini km wana njaa, haamini km siyo wezi, haamini makabila yote yanastahili haki na huruma yake, haamini km Rais hunyenyekea na kulaumiwa.

Ilituweze kuzishiriki tabia hizi yatupasa tuwe "WAOGA" kupindukia, na uoga ni "dhambi" kwakua ni tabia ya shetani...! MUNGU huchukizwa na taifa la waoga na ataliangamiza taifa.

Tabia hizi ni za kiimla na udikteta unataka tuishiriki na rais? Taifa hili litadumu kweli ?

Kwa kuishiriki kwetu unataka tuuvae uhalisia kwamba sote tuwe na tabia ya udikteta .... yaani maana yake miongoni mwetu asitokee asiye kuwa na hulka ya udikteta... je taifa hili litakuwepo kwa kiila mtu kuto nyenyekeana kuheshimiana, kuaminiana na kutokua na makubaliano zaidi ya maoni yako binafsi km ilivyokua BABELI ( watu hawakuweza kuendelea kujenga mnara baada ya kuuvaa ukabila, umimi na yote kama yafanyikavyo hapa kwetu)? Tabia hii si ya kuigwa hata kidogo.

Kama taifa linaloishi tunatakiwa tuwe na tabia za kiungu ( MUNGU) tupendane, tumwogope MUNGU tu! wengine wote tuheshimiane, tuuthamini na kuuenzi uumbaji yaani binaadam mwenzio... ! Tabia hizi ni za uhai kwasababu zinatoka kwa MUNGU kiini cha uhai .... ndio tuzishiriki.

Lakini udikteta ni tabia ya shetani hatuwezi kushiriki tabia hizi au tukubaliane kuliua taifa hili kwa kushiriki ufedhuli wa aina hii "uoga"
 
Sijui nchi za Africa zina mzimu gani katufungia kabisaa
 
Back
Top Bottom