Mkuu wa Mkoa wa Singida aagiza kukamatwa kwa waliotafuna mishahara hewa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe ameagiza mamlaka zinazohusika kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu watakaobainika kutafuna fedha za mishahara hewa kabla ya mwezi huu kumalizika.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo juzi kwenye kikao cha kufahamiana kilichohudhuriwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa idara ya sekretarieti ya mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ofisini kwake.

Katika hotuba yake, alisema uhakiki uliofanyika hivi karibuni mkoani humo ulibainika kuwa na wafanyakazi hewa wengi, jambo linaloonyesha kuwapo kwa ubadhirifu wa kiwango cha juu cha fedha za umma.

“Naagiza kila mmoja wenu akaangalie kwenye taasisi yake iwapo wafanyakazi wanaolipwa mishahara ndiyo hao waliopo kazini au la. Kuna madai wastaafu, waliohama na hata watumishi waliokufa mishahara yao bado inalipwa hadi hivi leo,”alisema.

“Iwapo itagundulika kuwa kuna watu walioshiriki katika ulaji huo wa fedha za umma, wakamatwe mara moja ifikapo Aprili Mosi, mwaka huu na kufikishwa kunakohusika haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.”

Mtigumwe aliwakumbusha viongozi hao umuhimu wa watumishi walio chini yao kufanya kazi kwa uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

“Haiwezekani mtu atoke kijijini kisha arudi bila kuhudumiwa, lazima kuwahi kazini na kukaa hadi mwisho wa saa za kazi,” alisema.

Pia, alisisitiza umuhimu wa kila taasisi ya Serikali mkoani humo kufungua kitabu cha kero za wananchi na kuhakikisha zinaorodheshwa na kuonyesha hatua halisi iliyofikiwa katika kuzishughulikia.
 
Hewa inapofukuza hewa....Wind is air in motion from high pressure to low pressure area....haya yanafanyika kwa mashinikizo ya kuhalalisha uwepo wao...uchaguzi wenye matokeo hewa ya kupika huzaa viongozi hewa...hivi nani asiyejua hapa tuna mfunika mdudu ndani ya kidonda badala ya kumuua...nakumbuka tangu enzi za fagio la chuma kila serikali mpya imekuwa ikija na mwembwe hizi mwisho wa siku tunaambulia kulia maana badala ya kuondoa mizizi tunapukutisha matawi...yanayokuja kuchipuka yanakuwa bora kuliko ilivyo sasa.....kura hewahuhuzaa watumishi hewa hewa inakuwa nzuri kwa wenzenu ila kwenu mbaya....kama mnayo nia ya dhati msingefanya maigizo hewa ya chaguzi hewa kwenye halmashauri nyingi na baadhi ya majimbo na hususan Zanzibar....tuepuke hewa kona zote kama taifa tuache ushabiki
 
Yale maigizo ya uchaguzi Zbar vipi? Naona jumuia ya ulaya na marekani wamesusa sherehe za kuapisha maigizo ya ccm
 
Safi sana mkuu wa mkoa Mungu akubaliki sana na akupe nguvu za kupambana na mafisadi
 
Back
Top Bottom