Mkuu wa mkoa wa Mwanza, aagiza Mganga mkuu wa Wilaya aondolewe katika nafasi yake

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Mkuu wa mkoa wa MWANZA MAGESA MULONGO ameagiza mganga mkuu wa wilaya ya MAGU Dr.NICKSON ITOGOLO na katibu wa hospitali ya wilaya hiyo
image.php

Mkuu wa mkoa wa MWANZA MAGESA MULONGO

Mkuu wa mkoa wa MWANZA MAGESA MULONGO ameagiza mganga mkuu wa wilaya ya MAGU Dr.NICKSON ITOGOLO na katibu wa hospitali ya wilaya hiyo MICHAEL NDALAWA kuondolewa kwenye nafasi zao kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ya kazi.

MULONGO ametoa agizo hilo baada ya viongozi hao kushindwa kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya wahudumu wa afya na wauguzi 70 ambao michango yao haijawasilishwa kwenye mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii NSSF kwa muda wa miaka minane.

Hayo yamejiri siku chache baada ya wahudumu wa afya wa hospitali ya wilaya ya MAGU mkoani MWANZA kumlalamikia mwajiri wao kwa kushindwa kuwasilisha michango yao katika mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii NSSF.

Akizungumza kwenye kikao na waandishi wa habari mjini mwanza MULONGO ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya viongozi wanaosimamia sekta ya afya wilayani magu kushindwa kupata ufumbuzi wa malalamiko ya wafanyakazi hao kwa muda wa miaka minane.

Tarehe 29 December 2015

Na AMICUS BUTUNGA wa TBC
 
Anayepaswa kuwajibishwa ni afisa utumishi wa halmashauri kuliko hao walioowajibishwa
 
Mwaka huu tutaona na kusikia mengi,utakuta mkuu wa mkoa hana hata utaalamu wa matibabu.
 
Anayepaswa kuwajibishwa ni afisa utumishi wa halmashauri kuliko hao walioowajibishwa
Kutoka upishi mpaka ukuu wa mkoa unategemea atajua nini ukimwambia akwambie job description ya DMO,RMO, ndo utacheka ufe...
 
Mimi nilikuwa ninadhani kwamba mwenye mamlaka ya kufukuza madaktari wa mikoa na wilaya ni waziri wa afya! Kumbe hata mkuu wa mkoa anaweza fanya hivyo! Isije ikawa jamaa amevuka mpaka wa mamlaka yake.
 
Fukuza fukuza ya bila mpango hii itamaliza watumishi,wengine wanafanya kazi kwa visasi tu
 
Back
Top Bottom