Mkuu wa mkoa na Rais wetu

Negan The Dead

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
340
994
Habari zenu Wakuu
Nimekua msomaji kwa muda wa miaka 10 ila leo nimeamua kuchangia maana hii imenigusa sana.

Kuna msemo usemao uzoefu ni mwalimu mzuri sana , ila kuupata inahitaji uwe na cheti cha taaluma fulani.Siwezi kupinga kua mkuu wa mkoa wa Dar alikua na point ya msingi sana katika hoja yake ya madawa ya kulevya.Hakuna anaepinga kua madawa ya kulevya yana madhara makubwa sana kwa mwanadamu. Mfano ni rahisi sana kwa mateja tunaowaona kwenye vituo vya magari, tulio jirani nao na hakuna anaepinga kua hii vita ni ya dunia nzima.

Labda nitoe historia fupi ya madawa ya kulevya, dawa hizi kama morphine, cocaine na heroin zilikua ni legal (bali alcohol au pombe ilikua ni illegal kwa sababu tuu watu walikua wanapiga wake zao wakilewa) kutumika mwanzoni mwa miaka ya 1920.Mfano cocaine au mti wa raha ulitumika kipindi cha vita ya kwanza ya dunia kufanya informal operation mara mtu anapojeruhiwa.Baada ya vita ya kwanza ya dunia watu wakawa wanatumia madawa haya kwa starehe zao.Tatizo kubwa lilikua ni kwenda kazini maana mtu alikua anatumia madawa wiki nzima.Hili lilikua tatizo hivyo dunia ikaamua madawa yawe illegal kwa sababu watu hawaendi kazini sio kiafya.Kuziba pengo la starehe watu wakaruhusu Pombe iwe legal, sababu mtu akilewa, anaweza piga mke wake ila kesho yake akawa kazini asbuhi na mapema.Kuhusu kupiga mke wakatunga sheria kali za kijinsia kuzuia au kupunguza unyanyasajia wa wanawake na watoto.

Baada ya hiyo taarifa fupi nirudi kwetu hapa Dar, kwa mkuu wetu wa mkoa ambaye anapendwa sana na mtukufu rais. Mkuu wa mkoa ameanzisha vita ya madawa ya kulevya mara baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka, kwa nini??Isitoshe matokeo hayo Dar es salaam, ambapo kuna resources nyingi na huduma nyingi za masomo ya ziada kuna shule zaidi ya tano zimeshika mkia, kwa nini?Halafu taarifa zimekuja kua mkuu wetu wa mkoa, alipata sifuri kwenye mtihani wake wa kidato cha nne.Hakuna uchunguzi kutoka taasisi za kiserikali kua hizo tuhuma ni kweli au la, hakuna uchunguzi kwa nini shule zilizoshika mkia zinatoka Dar wakati kuna vitu vingi vya kumfanya mwanafunzi apate daraja la kwanza achilia mbali la tatu, pili na nne.

Kama nilivyosema awali, vita ya madawa ya kulevya ni endelevu na naiunga mkono 100%.Mkuu wetu wa mkoa alitakiwa ajibu hoja kwa nini anatumia cheti cha mtu ambapo ni kosa kisheria.Vile vile serikali ilitakiwa kujibu hoja kwa nini Mkuu wa mkoa ameendelea kua mkuu wa mkoa mpaka sasa.Sidhani kama ni kitu kigumu kama vitu vyote vipo ubaoni.

Mheshima na mtukufu na mtu aisepangiwa vitu rais wetu angetujibu sisi hohehahe kwa nini Mkuu wetu wa mkoa mpaka sasa yupo pale bomani.Ni hoja tu na tuna haki ya kumuuliza kwa sababu aliingia madarakani kwa kura sio mtutu wa bunduki.Mambo ya kusema hapangiwi kitu, au yeye ndio kila kitu haimaanishi asijibu hoja zetu.Tafadhali mkuu wetu, nijibu hoja mbili tuu, kwa nini Mkuu wa mkoa wa Dar aendelee kuwepo hapo na kwa nini asichukuliwe hatua kwa kutumia cheti cha mtu.

Leo tumepata matokeo ya tume ya mh Nape Nnauye. Hebu tusaidie mkuu wa nchi kweli hakuna mtu mwenye uwezo zaidi ya D.A.B Tanzania nzima?Nimeangalia teuzi zako nyingi na umeweka wasomi kweli kweli PHD , PROF n.k. Kwali elimu ya mkuu wa mkoa inatosha kuongoza sehemu ambayo yawezekana inatoa wasomi wengi Tanzania?

Ahsante sana.
 
Umenikumbusha fact nyingine....
Daud bashite baada ya matokeo ya form4 kutoka na kuwa mabaya....akaanzisha vita ya madawa kwa lengo la kua watu watazungumzia maswala ya elimu kwa upana....elimu ambayo yeye binafsi ilimsumbua....akatafuta pakutokea...bahati mbaya hata kivuli alichokimbilia cha madawa ya kulevya bado aliumbuka.

Conclusion
Hata mkuu wa mkoa asingeanziasha vita ya madawa bado maswala ya vyeti yangerise kwenye mjadala wa kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
 
Mimi ni rais ninayejiamini. Mawazo yangu ni kwamba tusipoteze mda kwenye mambo ya udaku. Yasitutoe kwenye direction. Makonda wewe chapa kazi. Hakuna wa kunipangia Kwa sababu hata fomu nilichukua mwenyewe
 
Aweke vyeti mezani! Inakuaje unanunua cheti cha MTU unabadilisha mpk jina lako la asili? Kwa mini asirisiti?
 
Habari zenu Wakuu
Nimekua msomaji kwa muda wa miaka 10 ila leo nimeamua kuchangia maana hii imenigusa sana.

Kuna msemo usemao uzoefu ni mwalimu mzuri sana , ila kuupata inahitaji uwe na cheti cha taaluma fulani.Siwezi kupinga kua mkuu wa mkoa wa Dar alikua na point ya msingi sana katika hoja yake ya madawa ya kulevya.Hakuna anaepinga kua madawa ya kulevya yana madhara makubwa sana kwa mwanadamu. Mfano ni rahisi sana kwa mateja tunaowaona kwenye vituo vya magari, tulio jirani nao na hakuna anaepinga kua hii vita ni ya dunia nzima.

Labda nitoe historia fupi ya madawa ya kulevya, dawa hizi kama morphine, cocaine na heroin zilikua ni legal (bali alcohol au pombe ilikua ni illegal kwa sababu tuu watu walikua wanapiga wake zao wakilewa) kutumika mwanzoni mwa miaka ya 1920.Mfano cocaine au mti wa raha ulitumika kipindi cha vita ya kwanza ya dunia kufanya informal operation mara mtu anapojeruhiwa.Baada ya vita ya kwanza ya dunia watu wakawa wanatumia madawa haya kwa starehe zao.Tatizo kubwa lilikua ni kwenda kazini maana mtu alikua anatumia madawa wiki nzima.Hili lilikua tatizo hivyo dunia ikaamua madawa yawe illegal kwa sababu watu hawaendi kazini sio kiafya.Kuziba pengo la starehe watu wakaruhusu Pombe iwe legal, sababu mtu akilewa, anaweza piga mke wake ila kesho yake akawa kazini asbuhi na mapema.Kuhusu kupiga mke wakatunga sheria kali za kijinsia kuzuia au kupunguza unyanyasajia wa wanawake na watoto.

Baada ya hiyo taarifa fupi nirudi kwetu hapa Dar, kwa mkuu wetu wa mkoa ambaye anapendwa sana na mtukufu rais. Mkuu wa mkoa ameanzisha vita ya madawa ya kulevya mara baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka, kwa nini??Isitoshe matokeo hayo Dar es salaam, ambapo kuna resources nyingi na huduma nyingi za masomo ya ziada kuna shule zaidi ya tano zimeshika mkia, kwa nini?Halafu taarifa zimekuja kua mkuu wetu wa mkoa, alipata sifuri kwenye mtihani wake wa kidato cha nne.Hakuna uchunguzi kutoka taasisi za kiserikali kua hizo tuhuma ni kweli au la, hakuna uchunguzi kwa nini shule zilizoshika mkia zinatoka Dar wakati kuna vitu vingi vya kumfanya mwanafunzi apate daraja la kwanza achilia mbali la tatu, pili na nne.

Kama nilivyosema awali, vita ya madawa ya kulevya ni endelevu na naiunga mkono 100%.Mkuu wetu wa mkoa alitakiwa ajibu hoja kwa nini anatumia cheti cha mtu ambapo ni kosa kisheria.Vile vile serikali ilitakiwa kujibu hoja kwa nini Mkuu wa mkoa ameendelea kua mkuu wa mkoa mpaka sasa.Sidhani kama ni kitu kigumu kama vitu vyote vipo ubaoni.

Mheshima na mtukufu na mtu aisepangiwa vitu rais wetu angetujibu sisi hohehahe kwa nini Mkuu wetu wa mkoa mpaka sasa yupo pale bomani.Ni hoja tu na tuna haki ya kumuuliza kwa sababu aliingia madarakani kwa kura sio mtutu wa bunduki.Mambo ya kusema hapangiwi kitu, au yeye ndio kila kitu haimaanishi asijibu hoja zetu.Tafadhali mkuu wetu, nijibu hoja mbili tuu, kwa nini Mkuu wa mkoa wa Dar aendelee kuwepo hapo na kwa nini asichukuliwe hatua kwa kutumia cheti cha mtu.

Leo tumepata matokeo ya tume ya mh Nape Nnauye. Hebu tusaidie mkuu wa nchi kweli hakuna mtu mwenye uwezo zaidi ya D.A.B Tanzania nzima?Nimeangalia teuzi zako nyingi na umeweka wasomi kweli kweli PHD , PROF n.k. Kwali elimu ya mkuu wa mkoa inatosha kuongoza sehemu ambayo yawezekana inatoa wasomi wengi Tanzania?

Ahsante sana.
Jibu ni rahisi tu usiumize kichwa ndugu yangu juu ya kwa nini Rais hajaweza kumwondoa Makonda. Hajawahi kutokea mtu aliyejitosa kupambana na madawa ya kulevya wazi wazi kama yeye. Siku hizi tunaongelea hii vita kwa sababu yake. Makonda ni jasiri, shupavu na mchapa kazi. Tumsamehe pale alipokosea na yeye pia asione shida kuomba radhi. Ni jambo la kawaida kukosea.
 
Sikatai wala kupinga ujasiri wake .Swali langu kubwa ni kwamba kwa nini hajibu tuhuma zinazomkabili??
 
Back
Top Bottom