Chikumba one
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 1,009
- 1,642
Kuna juhudi kubwa zinafanyika kuwahamasisha Wananchi kesho waache shughuli zao na kukaa mbele ya luninga kufuatilia matangazo ya moja kwa moja ya makabidhiano ya ripoti ya pili ya tume iliyoundwa juu ya sakata la mchanga wa Dhahabu!
Mkuu wa mkoa mmoja usiku huu ametoa gari la matangazo linapita mitaani kuhamasisha umma kufuatilia tukio hilo bila kukosa!
Sina tatizo na juhudi hizi za Mkuu wa mkoa, tatizo langu ni nini hasa malengo ya jitihada hizi?
Yapo maswali mengi yanajitokeza, kwa nini jitihada hizi hazipo kwenye kuwataka Wananchi wafuatilie mijadala ya bungeni?
Kwa nini jitihada hizi zisifanywe kwa kuwataka Wananchi waulizie ilipo mikataba mbalimbali iliyopelekea Taifa kupata hasara kubwa katika sekta mbalimbali?
Kwa nini Wananchi wanatakiwa waache kazi zao kufuatilia makabidhiano ya ripoti hii badala ya umma kuelezwa ni kina nani waliolifikisha hapa Taifa hili?
Je, maelekezo haya yametolewa kwa wakuu wote wa mikoa? Kama jibu ni ndiyo, lengo hasa ni lipi?
Je, kuna nini 'special' katika ripoti hiyo?
Je, hii ripoti tayari inajulikana kwa wakubwa kiasi cha kutaka umma uhamasishe kuifuatilia?
Siamini serikali inaweza kufanya uhamasishaji mkubwa kiasi hiki pasipo kujua kilichomo ndani ya ripoti!
Lkn swali muhimu kabisa ni hili, Je, kipi muhimu kwa Umma kukijua kati ya ripoti hii na mikataba inayoleta matatizo yote haya?