figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Sera ya elimu bure nchini imeshishindwa kueleweka vizuri mjini Songea mkoani Ruvuma ambapo wananchi katika kata ya mfaranyaki mjini Songea wamegoma kuchangia michango katika kikao kilichoitishwa na diwani wa kata hiyo kwa ajili ya kuwataka kuchangia michango ya chakula na mlinzi katika shule ya msingi Misufini na hivyo kuzusha vurugu kubwa.
Vurugu hizo zilitokea baada ya diwani wa kata ya Mfaranyaki kwa tiketi ya Chadema Bw. Seneta Yatembo kuitisha mkutano wa wazazi kuchangia michango ya chakula na mlinzi shuleni ambapo diwani huyo na mwenyekiti wake wa Chadema wilaya ya Songea Bw. John Mwankina wametofautiana katika suala hilo.
Baada ya maelezo hayo ya diwani ndipo zikafuata vurugu kubwa za wananchi wakiimba hawataki michango na kubishana na diwani huyo wakati akihutubia ambapo wananchi nao wakagawanyika katika suala hilo.
Chanzo: ITV