Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhan ajibu taarifa za upotoshaji matokeo ya Dimani

Kinjekitile junior

JF-Expert Member
Apr 20, 2015
4,404
581



Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa Kura 234 ziliharibika katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani, Zanzibar Januari 22, 2017.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Ramadhan Kailima amesema kuwa Wapiga Kura walioandikishwa katika jimbo la Dimani, Zanzibar ni 9,275.

Amesema kati ya hao wapiga Kura 6,406 walijitokeza kupiga Kura siku hiyo ambapo Kura halali zilikuwa 6,172 na Kura zilizoharibika zilikuwa 234.

Mkurugenzi Kailima ameeleza kuwa katika Uchaguzi huo vyama 11 vilikuwa na wagombea wa Ubunge ambapo Chama cha ACT-Wazalendo kilipata Kura 8, Chama cha ADC Kura 42, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kura 4860, CHAUMA Kura 10, Chama Cha Wananchi CUF Kura 1234, Chama cha DP Kura 8.

Vingine ni Chama cha NRA kura 1, SAU Kura 4, TLP kura 2, Chama Cha UMD Kura 2 na Chama Cha UPDP Kura 1 na kufanya jumla ya Kura za Vyama vyote kuwa 6172.
 
Back
Top Bottom