Kambi hiyo ya uchunguzi na matibabu ya kibingwa bobezi inayofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Vodacom Foundation Tanzania imeanza leo Machi 10, 2026 ambapo huduma za uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti, saratani ya tezi dume, magonjwa ya uzazi na kina mama, masikio, pua,koo meno na magonjwa ya Watoto zinafanyika bila malipo.