Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Zantel apigwa risasi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Hii imetokea barabara ya Coca Cola karibu na Nabaki Afrika. Inasemekana director huyo anajulikana kwa jina la Gabriel Kamukara amepoteza maisha kwenye eneo la tukio.

Inasemekana alikuwa na kiasi cha pesa na hao majambazi wamefanikiwa kuzichukua.

Watu 2 wamepigwa risasi na kuporwa fedha wakiwa katika gari lao eneo la Nabaki Afrika DSM.


===========================

Mfanyakazi wa Zantel auawa kwa kupigwa risasi
Gabriel+PGOTO.jpg

Aliyekuwa Meneja wa operesheni wa kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Zantel, Gabriel Rafael wakati wa uhai wake
Dar es Salaam. Meneja wa operesheni wa kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Zantel, Gabriel Rafael ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.

Tukio hilo limetokea jana saa 4:45 asubuhi eneo la ofisi za kampuni ya Nabaki Afrika, iliyopo Mwenge, mita chache karibu na kampuni ya Coca-Cola.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema haikujulikana mapema meneja huyo alikuwa akitokea wapi na gari lake aina ya Toyota Double Cabin.

Alisema baada ya kupata taarifa za mtu kuuawa kwa kupigwa risasi, polisi walifika eneo la tukio na kubaini kuwa meneja huyo alikuwa amepigwa risasi kwenye kwapa la mkono wa kulia.

Kamanda Wambura alisema ndani ya gari la mfanyakazi huyo walikuta simu, laptop na fedha taslimu Sh1 milioni.

“Mwili wake umepeleka kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo pamoja na kuwasaka waliofanya mauaji hayo,” alisema Wambura.

Taarifa za mauaji ya meneja huyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana mchana zikieleza kuwa, alikuwa akitokea benki kuchukua fedha.

Katika hatua nyingine, Wambura alitoa rai kwa wakazi wote kutumia njia za kiteknolojia kuchukua na kuhifadhi fedha badala ya kutembea nazo mfukoni.

Chanzo: Mwananchi

 

Attachments

  • IMG-20151228-WA0018.jpg
    IMG-20151228-WA0018.jpg
    111.8 KB · Views: 887
Last edited by a moderator:
Hii imetokea barabara ya Coca Cola karibu na Nabaki Afrika. Inasemekana director huyo anajulikana kwa jina la Gabriel Kamukara amepoteza maisha kwenye eneo la tukio.
Pole sana wafiwa! Alikuwa amebeba pesa? Chanzo ni nini?

Hivi huwa una camera ya kunasa matukio ya ajali na majanga?
 
Hii imetokea barabara ya Coca Cola karibu na Nabaki Afrika. Inasemekana director huyo anajulikana kwa jina la Gabriel Kamukara amepoteza maisha kwenye eneo la tukio.

Mkuu,
Leo haukufanikiwa kupata picha!?
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala Pema Peponi ....Amina.
 
Haya majambazi ni wazi yanakuwa na full info za hizo hela
 
Haya matukio yanazidi kuongezeka tu na bado sijasikia Mtumbuaji akiahidi kulala nayo mbele
 
Daah Brother G. Kamukara umetutoka tayari, daah! Yaani kama muvi vile. Upumzike kwa Amani, Amina!

Ahsante!
 
Toka nimemuona yule jamaa anspigwa risasi kwenye gari pale TAZARA nimekosa amani na madereva wa bodaboda, nikiwa naendesha gari huwa nahisi inaweza kunitokea muda wowote

Alale pema huyo Ndugu yetu
 
Back
Top Bottom