KingJoh
Member
- Oct 20, 2019
- 12
- 11
Ni matumaini yangu kuwa Mungu yu pamoja nanyi akiwalinda ili kutekeleza majukumu ya kila siku.
Nadhani ni vyema nikienda moja kwa moja kwenye mada.
Itakumbukwa kuwa, hapo jana wakati Mh Rais akiwaapisha Mawaziri na Manaibu, aligusia kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea katika Halmashauri ya Geita na Manispaa ya Mpanda yamkini yakiongozwa na Wakurugenzi wenyewe. Hii ni hatua nzuri sana na nipongeze kwa Serikali inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuliona hilo.
Lakini nipende kutoa taarifa ya kuwa, kuna Halmashauri inaitwa Mpanda Vijijini au Tanganyika, kuna uozo uliopitiliza kufikia kiwango kwamba, wananchi wanahisi Mkurugenzi anatumia dawa wakiangalia wengine wakitumbuliwa kwa makosa madogo kuliko yeye unayoyafanya lakini bado hajaingia anga za Mh Rais.
Niseme tu ukweli mkurugenzi huyu anayeitwa Romuli ni jipu na ndiye mpinga maendeleo NO1 kwa wilaya ya Tanganyika.
1. Ikumbukwe kuwa Waziri Mkuu aliutembelea mkoa wa katavi mwaka huu, na akapita eneo la karema akikagua maendeleo ya ujenzi wa bandari ya karema. Alipata fursa ya kuwahutubia wananchi wa maeneo ya karema na moja ya point aliyoisema, ilihusu kujengwa kwa shule ya sekondari isengule kwa kutumia hela zilizopatikana kwa kuuza magogo ambayo yalitaifishwa na serikali na ilitarajiwa ujenzi wa hiyo shule sambamba na ujenzi wa hospitali na fedha tukaambiwa zipo. Cha kushangaza, miradi hiyo wala haiendelei kwa kile kinachodaiwa kuwa hela imeshapigwa na wajanja wa mjini wakiongozwa na mkurugenzi.
2. Mkurugenzi amekuwa akifanya re-allocation hela za watumishi kwa matumizi ya kipuuzi kabisa. Kwamfano, kuna hela ya kujikimu ilitumwa na serikali kwa ajili ya walimu intake ya mwaka jana mwezi wa nne kama sikosei, mkurugenzi alizichukua na kuzinunulia mafuta ili afanye ziara zake ambazo ofcoz znaweza kuwa na tija lkn tatizo ni, hakuonai
huruma kwa hao walimu ambao walikuwa katika hali mbaya kiuchumi?? Lkn pia, kuna walimu wameajiriwa mwaka 2017 mwezi wa nne, mpka leo hawajapewa hela za kujikimu ambazo wengine nchi hii wameshalipwa, kwanini halmashauri hii?
3. Kuna miungu watu kwny idara ya fedha pale halmashauri wakikingiwa kifua na mkurugenzi. Ni wadada wawili ambao wamekuwa na majibu mabaya sana kwa watumishi. Unakuta mwl mkuu anafuatilia hela kwa ajili ya shule, anatumia siku nne kukamilisha process na ukiangalia hakuna sababu ya msingi coz, halmashauri zinngne ambazo zipo karibu hawatumii muda wote huo. Kwnn halshauri hii?
4. Conclusively, hakuna alilolifanya kwa utawala wake.
Niiombe serikali, halmashauri hii, inatakiwa kukaguliwa pia na kwa mimi ninavyoona, hii ndio halmashauri yenye madudu kuliko halmashauri zote nchini.
Waziri nitafurahi sana kama utaipitia hii