Mkurugenzi TANTREAD usitupotoshe kuhusu Dar es Salaam International Trade Fair

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
23,251
Reaction score
28,406
Leo nimekusikia ukisema kwenye maonesho ya mwaka huu yatakayoanza 28/06 mpaka 12/07 (hivi kama sijakosea) mmepanga siku ya wanafunzi kuwafahamisha kuhusu Sabasaba ni nini!

Nilishituka kidogo kuhusu uhusiano gani uliyopo kati ya Sabasaba na maonesho hayo ya Dar es Salaam! Nijuavyo zamani chini ya mfumo wa chama kimoja Sabasaba ilikuwa ni sherehe ya kuzaliwa TANU na tarehe 07/07 ndiyo ilikuwa kilelele cha sherehe ambayo kwa Dar es Salaam yalifanyika maonesho ambayo baadae yakawa ya kimataifa.

Chini ya mfumo wa vyama vingi sherehe ya Sabasaba iliondolewa kwenye sherehe za taifa, lakini tarehe 07/07 ilibaki kuwa ni siku ya mapumziko ili watu watembelee maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam!

Japo wengine hatujui watu wa mikoani wanayatembelea vipi hayo maonesho! Sasa Mkurugenzi wa Tantrade sijui unataka kuwafundisha Sabasaba ipi hao wanafunzi maana hatumo tena kwenye mfumo wa chama kimoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…