Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Monduli ondoa hii Aibu

MLIMAU

Member
Feb 2, 2017
17
2
Mh. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Monduli nakuja tena kwako kukuomba umchukuliye hatua Mtendaji wa Kijiji cha Makuyuni kwa kukiuka maadali ya kazi yake na kujiingiza katika matendo ya kuwaonea wananchi huku akisukumwa na mwenyekiti wa Kijiji Mzee. Sule.

Jana tarehe 7/02/2017 Mtendaji huyu alitangaza na kuitisha mkutano wa wananchi wote kwa kutumia kipaaza sauti kujadili suala la fidia za maeneo unakopita Msongo wa KV 400 kuwa "fidia ya baadhi ya maeneo ya wananchi ipelekwe kwenye mfuko wa maendeleo ya Kijiji huku akijua sio utaratibu. Lengo ni lao liko palepale kuwa endapo itafanyika hivyo itakuwa rahisi kwao kuchota hizo hela kama walivyokwisha kudhamiria;. Wakati wakifanya hivyo wanajua kabisa wanaotakiwa kulipwa fidia hizo ni wananchi na taasisi ambazo tayari zilipewa umiliki na Kijiji na kuwa tayari wameleta malalamiko kwako Mkurugenzi.
Mkutano wa jana waliandaliwa wanakijiji wahuni na kupewa rushwa ya viroba na idadi yao hardly haikufika 50. Wakati walioandaliwa kusema ndiyoooo kwenye mkutano wakiunga mkono maazimio hayo kuwa BAADHI ya wenye maeneo wanyang'anywe fidia ielekezwe kwenye mfuko wa Kijiji, Maeneo ya Kijiji waliosimama Ma Afisa Tarafa, na Mwenyekiti wa Kijiji hayataguswa na maazimio ya mkutano huo.

Leo tarehe 8/02/2017 tayari Mtendaji wa Kijiji cha Makuyuni anatengeneza Muhtasari ili auwasilishe kwako Mkurugenzi kukudanganya kuwa kilichoko ni maazimio ya Kijiji. Lakini maazimio hayo hayagusi fidia itakayolipwa maeneo ya Mwenyekiti wa Kijiji wala Ma afisa tarafa licha ya kwamba yote kuwa ndani ya ardhi ya Kijiji. Huu ni ubaguzi na lazima Mtendaji aeleze ni vigezo gani alivyotumia kusema fidia ya huyu iende mfuko wa maendeleo ya Kijiji na hii wapewe waliosimama.

Mkurugenzi utaletewa Mhustasari huo leo au kesho na Mh. tunaomba busara zako zitumike kwani tunajiuliza kwanini Kijiji kitake kuchukua fidia kwenye maeneo ambayo tayari wamewamilikisha watu kwa barua bila idhini ya waliomilikishwa na bila kuwashirikisha katika jambo lolote. Hivi eneo alilomilikishwa mtu kwa taratibu zote za Kijiji iweje leo Kijiji kilivamie kwa interest za viongozi wa Kijiji ?

Hili likiachwa nia aibu kubwa kwa serikali ambayo ina viongozi makini. Tunatarajia kuwa huyu Mtendaji Mzee Mwenda anayevuruga eneo la Makuyuni hataachwa kuendelea kuwavuruga wananchi na kufanya atakavyo bila sheria kuchukua mkondo wake. Hili liko kwenye uwezo wa Mkurugenzi kwani ushahidi upo wazi kwa kila kitu.

Wananchi na taasisi ambazo fidia zake zinataka kuwa relocated ni wale waliotuma malalamiko kwa Mkurugenzi na kwa Wilaya lakini eti Mafisa Tarafa na wenyeviti waliosiamama na kudai fidia maeneo hayo hayo haswa ya barabara ya kuelekea Babati wao watalipwa. Hii ni double standard na Mkurugenzi anatakiwa aingilie huu mkutano BATILI wa jana(7/02/2017) kwani ungetakiwa ufanywe tangu wakati wa survey na ujumuishe pia wenye maeneo husika kama umefanywa kwa nia njema,na si huu uhuni uliofanywa jana na Mwenda.

Tunataka kuhisi kuna mtu au watu wako behind hii move " wanafanya "desperate attempt" kuwadhulumu wenye maeneo husika kwa kigezo kuwa sio wenyeji.

Mkurugenzi na serikali ya Wilaya tunakuomba kuondoa hii aibu kwani hili ni suala lililoko ndani ya uwezo wako na siamini kama utaruhusu uonevu wa namna hii kuendelea ukijua watanzania wote wana haki sawa.
 
Hivi kuna kitu kama hicho naomba wanasheria mtupe mwongozo kwenye hili
 
Mimi nilishakuwa mhanga kwenye mambo ya ardhi na nikiona kitu kama hiki huwa naona kama ni mimi naonewa
 
Huyu mkurugenzi atakuwa mvumilivu kama Mungu kwani huyu mtendaji anakaribia kumwingiza kiatu kichafu kinywani
 
Sikio la kufa halisikii dawa yaani hapa labda wamsubiri tu Rais akiwa na mkutano wakaingie kama yule mama Mjane
 
Malalamiko haya yamezunguka huku almost mwezi sasa ilitakiwa huyu mtendaji awe anadeki rumande.
 
Hivi kusema mtu amepoteza uaminifu wa kuutumikia umma kuna zaidi ya hapo. kama unakaa mahali watu wanalia badala ya kufurahi basi uko mahali ambapo sipo
 
Ninatarajia kuwa mkurugenzi na Mkuu wa wilaya wanamsubiri Mwenda na timu yake ili wakifika tu waelekezwe sehemu inayowahusu. haiwezekani watu wanaleta malalamiko halafu serikali ya Kijiji inapambana kuyapangua huku uongozi wa wilaya wakijua ukweli uliko. Ni ushahidi gani wanataka tena ?
 
Mbaya zaidi wanaolalamika hawakutanishwi na serikali ya Kijiji bali mkurugenzi amekuwa akiwasiliana na Serikali ya Kijiji tu several times in absence ya walalamikaji
 
Mbaya zaidi wanaolalamika hawakutanishwi na serikali ya Kijiji bali mkurugenzi amekuwa akiwasiliana na Serikali ya Kijiji tu several times in absence ya walalamikaji
Kuna dalili ambazo siyo nzuri kwa hiyo lazima watu walalamike kama kunasuluhisha kwa kusikiliza upande mmoja kuna tatizo
 
Labda serikali inataka kuonyesha kuwa yenyewe ni Serikali inaweza kumfanya mwananchi chochote au Ku revoke chochote ili kurahisisha kesi.
 
Serikali kuu ikiamua ku side na Kijiji itakuwa LAANA na kwa viongozi husika na hapa ni hekima na busara zao tu ndizo zifanye kazi
 
Back
Top Bottom