Ni Bodi ya Kahawa mnafitiniana sana. Mnatumia fedha nyingi za umma kupiga umbea ofisini badala ya kazi?
?NDIO MLIOMFANYIA HAYA?
FA Mkurugenzi Bodi ya Kahawa avamiwa, aibiwa gari
SHARE BOOKMARK PRINT EMAIL RATING
NaDaniel Mjema, Mwananchi
Posted Jumatano,Oktoba9 2013 saa 11:23 AM
KWA UFUPI Wezi hao walifanikisha dhamira yao baada kumteka mfanyakazi wa ndani na kisha kumfunga kamba mikononi na vitambaa usoni. Gari lililoibwa ni Toyota Raum namba T643 CDZ rangi ya Bluu.
SHARE THIS STORY
10
2 1
Tweet Tweet
Recommend Recommend Share Share
Building a Radio Studio?
Broadcast studio Pro Radio Station Technology
Setup Advice, Design & Construction Turn-key Solutions from the Experts
Moshi. Watu wasiojulikana wamevamia nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa (TCB), Adolf Kumburu iliyopo Shanty Town, mjini Moshi na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi likiwamo gari.
Wezi hao walifanikisha dhamira yao baada kumteka mfanyakazi wa ndani na kisha kumfunga kamba mikononi na vitambaa usoni. Gari lililoibwa ni Toyota Raum namba T643 CDZ rangi ya Bluu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha jana kutokea kwa tukio lililofanywa kati ya saa 6.00 na saa 7.00 mchana.
Ni kweli, tukio limetokea na miongoni mwa vitu vilivyoibwa ni gari. Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na tunaendelea na uchunguzi, alisema Kamanda Boaz.
Kamanda Boaz ametoa wito kwa wananchi wenye taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na vitu vilivyoibwa waziwasilishe kwa siri kwake ama kwa maofisa wake na majina yatahifadhiwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kumburu alisema wezi hao walifanikiwa kuiba vitu mbalimbali na kuvipakia katika gari lake.
Mbali na gari hilo, pia televisheni aina ya Samsung Flat Screen, Deck aina ya Phillips, Micro-Wave, kompyuta mpakato aina ya Apple Mac Book, Samsung Min-Tablet na Digital kamera mbili pia viliibwa.
Kwa mujibu wa Kumburu, wezi hao huenda
walitumia mazingira ya ukimya katika eneo