Mkurugenzi halmashauri ya Malinyi akataa gari ya milioni 100, asema fedha zijenge zahanati

kisatu

Senior Member
Jan 16, 2015
151
225
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Malinyi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi,Marcelin Ndimbwa amemwandikia mwenyekiti wa Halmalmashauri Mh. Nasoro Liguguda na balaza lake, kubadilisha matumizi kiasi cha fedha shilingi milioni 100 alizotengwa kwa ajili ununuzi wa gari la mkurugenzi na kuzielekeza katika ujenzi wa Zahanati tatu.

Akizungumza na globu ya jamii ofisini kwake mapema leo asubuhi Ndimbwa amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya huduma za afya katika Wilaya hiyo kuliko yeye kununuliwa gari ya kifahari huku wananchi wakiwa wanateseka.

“nimemwandikia mwenyekiti wa Halmashauri barua juu ya kubadili matumizi ya fedha hizo kwani nimeona wazi kuwa mahitaji ya Zahanati katika wilaya yangu ni makubwa kuliko hiyo gari kwani Malinyi inahitajika kuwa na zahanati 33 lakini mpaka sasa zipo zahanati tisa tu jambo ambalo linawafanya watu kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya”amesema Ndimbwa.

Amesema kuwa ujenzi wa Zahanati hizo unaanza mara moja katika vijiji vilivyo ainishwa na tayari wananchi walishaanza kukusanya nguvu kwa kujitolea Mchanga ,Mawe na Matofali.

Ameweka wazi kuwa pindi ujenzi huo utakapoanza autasimama kwani kutokana na fedha hizo na nguvu ya wananchi iliyopo kila kitu kitakamilika kwa muda muafaka na wananchi watapata huduma kama ilivyo katika matarajio yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Nasoro Liguguda amesema kuwa ameridhia uamuzi huo kutokana na sera ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi kuitaka kila kata kuwa kituo cha afya na kila kijiji kuwa na zahanati moja kama mkurugenzi ameona gari sio ya muhimu na zahanati ndio ya msingi sisi tunashukuru.

Amesema kuwa wanampongeza mkurugenzi kwa uamuzi huo kwani ni viongozi wachache wenye kariba kama yake ya kufikiria wananchi kwanza kuliko yeye kwani angekuwa mwanasiasa ningeona kawaida lakini yeye ni mtendaji lakini bado amekuwa na uchungu na watu wa malinyi kuliko mtu mwingine yoyote hivyo sisi tunamuombea awe na moyo huohuo na aishi muda mrefu katika wilaya yetu.

Hakika Tanzania Mpya Inakuja kama viongozi sasa wameanza kuacha kujiangalia wenyewe kwanza
 
barite

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
228
225
Pongezi kwakwe,kwanza kule porini na ubovu wa miundombinu ya barabara hilo gari la kifahari lingekuwa mzigo mkubwa kwa wananchi,bora anunue landcruser mkonge any way kama ni nia yake nampa hongera ila kama ni kiki ya kupata ukuu wa mkoa au cheo kingine kikubwa anajidanganya kwani bwana yule hajaribiwi.
 
Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
159
250
Hongera sana ila isiwe mbinu ya kisiasa kutengeneza jina halafu ukipata wadhifa mkubwa uanze kutupiga hela maana sikuizi ukurugenzi ukiwa nzi wakijan tu tayar unasifa
 
Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,953
2,000
Hiyo sio suluhisho kwa matatizo ya wananchi bali kuhairisha tatizo.Akija Mkurugenzi mwingine atahitaji kununuliwa.
Suluhisho ni kuwa na mfumo mzuri wa mgawanyo wa keki ya Taifa.Sio kama ule tuliona mishahara minono na Posho kedekede kwa baadhi ya watu mfano wabunge kama tulivyoona katika tangazo la Zitto.
 
kisatu

Senior Member
Jan 16, 2015
151
225
Hiyo sio suluhisho kwa matatizo ya wananchi bali kuhairisha tatizo.Akija Mkurugenzi mwingine atahitaji kununuliwa.
Suluhisho ni kuwa na mfumo mzuri wa mgawanyo wa keki ya Taifa.Sio kama ule tuliona mishahara minono na Posho kedekede kwa baadhi ya watu mfano wabunge kama tulivyoona katika tangazo la Zitto.
Uongozi ni maono, hivyo uhalisia wa kiongozi ni kuwaweka mbele watu wake katika mazuri na nyuma katika mabaya tofauti na zamani ,pesa za kuwalipa wabunge kwenda ulaya kutembea na viongozi mbalimbali zilikuwepo lakini za kuwalipa MSD hospitali zipate dawa hazikuwepo
 
vesta

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
872
1,000

Ni kweli kabisa mkuu, lakini kwa kitendo alichofanya anahitahi kupongezwa. Ameona zahanati ni muhimu zaidi kuliko gari yake.
 
Amanijua

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,673
2,000
Tupo katika kipindi cha mpito na hizo ni mbinu za kutafuta umaarufu tu...

Katika vikao vya Halmashauri Mkurugenzi ni Katibu.

Mfumo ulipaswa kujua vipaumbele vya Halmashauri yao na siyo kuja kutuhadaa hapa
 
  • Thanks
Reactions: Nzi

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,953
2,000
Uongozi ni maono, hivyo uhalisia wa kiongozi ni kuwaweka mbele watu wake katika mazuri na nyuma katika mabaya tofauti na zamani ,pesa za kuwalipa wabunge kwenda ulaya kutembea na viongozi mbalimbali zilikuwepo lakini za kuwalipa MSD hospitali zipate dawa hazikuwepo
Hayo maono yake angeyaweka kwenye Sera.Hii ya kukataa fedha ni sawa na kumsaidia mgonjwa mmoja hela za Matibabu na kusahau kuna wengi wanaohitaji matibabu.
 
mgoloko

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
4,695
2,000
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Malinyi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi,Marcelin Ndimbwa amemwandikia mwenyekiti wa Halmalmashauri Mh. Nasoro Liguguda na balaza lake, kubadilisha matumizi kiasi cha fedha shilingi milioni 100 alizotengwa kwa ajili ununuzi wa gari la mkurugenzi na kuzielekeza katika ujenzi wa Zahanati tatu.

Akizungumza na globu ya jamii ofisini kwake mapema leo asubuhi Ndimbwa amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya huduma za afya katika Wilaya hiyo kuliko yeye kununuliwa gari ya kifahari huku wananchi wakiwa wanateseka.

“nimemwandikia mwenyekiti wa Halmashauri barua juu ya kubadili matumizi ya fedha hizo kwani nimeona wazi kuwa mahitaji ya Zahanati katika wilaya yangu ni makubwa kuliko hiyo gari kwani Malinyi inahitajika kuwa na zahanati 33 lakini mpaka sasa zipo zahanati tisa tu jambo ambalo linawafanya watu kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya”amesema Ndimbwa.

Amesema kuwa ujenzi wa Zahanati hizo unaanza mara moja katika vijiji vilivyo ainishwa na tayari wananchi walishaanza kukusanya nguvu kwa kujitolea Mchanga ,Mawe na Matofali.Ameweka wazi kuwa pindi ujenzi huo utakapoanza autasimama kwani kutokana na fedha hizo na nguvu ya wananchi iliyopo kila kitu kitakamilika kwa muda muafaka na wananchi watapata huduma kama ilivyo katika matarajio yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Nasoro Liguguda amesema kuwa ameridhia uamuzi huo kutokana na sera ya serikali na ilani ya chama cha mapinduzi kuitaka kila kata kuwa kituo cha afya na kila kijiji kuwa na zahanati moja kama mkurugenzi ameona gari sio ya muhimu na zahanati ndio ya msingi sisi tunashukuru.

Amesema kuwa wanampongeza mkurugenzi kwa uamuzi huo kwani ni viongozi wachache wenye kariba kama yake ya kufikiria wananchi kwanza kuliko yeye kwani angekuwa mwanasiasa ningeona kawaida lakini yeye ni mtendaji lakini bado amekuwa na uchungu na watu wa malinyi kuliko mtu mwingine yoyote hivyo sisi tunamuombea awe na moyo huohuo na aishi muda mrefu katika wilaya yetu.

Hakika Tanzania Mpya Inakuja kama viongozi sasa wameanza kuacha kujiangalia wenyewe kwanza
Naunga mkono haya ndiyo maendeleo tunayohitaji sio kujitazama kibinafsi wakati watu wanateseka kutafuta matibabu. Na hili liwe mfano kwa Pogba aachane na mpango wa kununua ndege wakati wananchi wana ukosefu wa mahitaji muhimu yakiwemo Afya, Ndege sio kipaumbele kwetu na kama kuna mahitaji hayo kwa mtu mmoja mmoja kuna mashirika mengi ya Ndege yapo Nchini na yanatoa huduma hiyo.
 
Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,953
2,000
Ni kweli kabisa mkuu, lakini kwa kitendo alichofanya anahitahi kupongezwa. Ameona zahanati ni muhimu zaidi kuliko gari yake.
Tukimpongeza atajisahau.
Anachotakiwa kuelezwa ni kuhamasisha watunga sheria ili waone umuhimu wa vipaumbele na sio ununuzi wa magari ya kifahari.
 
kisatu

Senior Member
Jan 16, 2015
151
225
Tukimpongeza atajisahau.
Anachotakiwa kuelezwa ni kuhamasisha watunga sheria ili waone umuhimu wa vipaumbele na sio ununuzi wa magari ya kifahari.
Baraza la madiwani ndio wenye maamuzi,hivyo tuhakikishe tunapata madiwani ambao ni people oriented katika kutafuta majawabu ya changamoto ndani ya jamii zinazotukabili kwa vipaombele
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom