Faru John II
Senior Member
- Dec 27, 2016
- 134
- 135
Imekuwa ni vigumu kwa Wanasiasa wengi kumtofautisha Freeman Aikaeli Mbowe yule Mwanasiasa ambaye wengi tunamfahamu na Freeman Mbowe kama mtu mwenye maisha binafsi ambayo hayafungamani kabisa na siasa anayoifanya.
Katika maisha ya Freeman Mbowe ambayo yako mbali kabisa na siasa watu wengi hawayajui sio Zitto Kabwe wala Tundu Lissu wala Mwanasiasa mwingine yoyote asiyekuwa sehemu ya familia ya Mbowe. Wanachotakiwa kujua akina Zitto na swahiba zake ni kuwa Mbowe ktk ulimwengu usiokuwa wa kisiasa ni kama Manji, kama Gwajima, kama Rostam, kama Ridhiwani, kama Chidi Benz, kama TID, kama Makonda, kama Sirro, kama Mengi au sawa na mtu yeyote yule anayeishi ktk ulimwengu wa tofauti na siasa. Hivyo anaishi maisha ya kawaida kama ya mimi nawewe.
Katika maisha haya ya kawaida, anakumbana na changamoto nyingi za maisha na anafanya analoona linaweza kutatua changamoto hizi kama ilivyo kwa mimi nawewe. Katika Mapambano dhidi ya dawa za kulevya serikali ikiwakilishwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam imejiridhisha kuwa Freeman Mbowe anatuhuma za kujibu katika jambo hili kama ilivyokuwa kwa Josephat Gwajima Gwajima na Yusuf Manji ambao ni watu wakubwa ktk jamii na wanaheshima zao pia lakini kwa kujiamini kuwa ktk maisha yao binafsi ni wasafi ndio maana wameitikia Wito wa serikali.
Mbowe na Wanasiasa wenzao akina Joseph Msukuma, Zitto Kabwe na wengine wa sampuli hiyo wanataka kutuaminisha kuwa ni makosa kwenda kupima Ukimwi kwa kiongozi wa dini na jaribio lolote la kuwapima Ukimwi viongozi wa dini ni matusi makubwa kwa waumini wao. This is mental slavery
Njia pekee ya kuwa-prove wrong wanaokudhania kuwa unaukimwi nawewe unajiamini huna Ukimwi ni kujitokeza ANGAZA sio kwenye vyombo vya habari na kuitisha Press Conference.
Niliunga mkono wabunge waliokuwa wakihoji kwa jazba kuwa kwanini Makonda anataja majina ya Vidagaa na anaogopa kuwa taja Mapapa wa Unga au Watu wakubwa wanaojihusisha na biashara ya Mihadarati, cha ajabu Makonda ameanza na baadhi yao, wabunge hao hao bila aibu wakaanza kuhamaki na kutoa mapovu yenye Ukubwa tofauti tofauti dhidi ya RC Makonda.
Binafsi naunga mkono ushauri wa Waziri Nape kuwa kuna haja ya kuendesha zoezi hili huku tukizingatia kutoharibu heshima waliojijengea watuhumiwa kwani hii itasaidia kutunza heshima zao endapo wanatuhumiwa kimakosa. Lakini naomba kumshauri Waziri Nape, Mwigulu Nchemba na wengine kuwa kazi yao sio kumshauri tu Makonda, kazi yao ni kushirikiana na yeyote aliye kwenye Mapambano haya kwa vitendo nasio maneno matupu ya kusifu na kupongeza na kukosoa. Wamuonyeshe Makonda kwa vitendo kuwa ushauri wao una matunda mazuri kwa kulifanya zoezi kuwa la Nchi nzima.
Orodha ya Chadema ya List of Shame pale Mwembeyanga Dar es Salaam iliwataja mafisadi wakubwa ktk Nchi hii kama Lowassa, Kikwete, Rostam nk ilivyotumika Approach hii ya kuwataja hadharani Mbowe, Tundu Lissu pamoja na Zitto hawakuona kama wanaharibu heshima ya watu, leo ametajwa Mbowe hadharani wao wanaona kadhalilishwa. Mimi wakati mwingine huwa napata wasiwasi watu wa sampuli hii kuwa Wapinzani au Wagizani. Hawaeleweki maneno yao.
Ushauri wangu kwa Makonda ni kuepuka kuwa mwongeaji sana kwenye social networks kwani sisi shida yetu sio maneno yake wala vifungu anavyotoa kwani tunavijua, shida yetu sisi ni Moto uzidi kuchoma kwa nguvu zote. Hivyo vifungu atafute sehemu sahihi ya kuvitolea, sisi tunachokitaka ni kazi tu kwani kazi ndio iliyomfanya apate ajira sio kujua vifungu vingi.