Mkosamali na Taasisi ya Urais

Mkosamali na Taasisi ya Urais

Kowalski

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Posts
348
Reaction score
111
Mkosamali>> Kwanini Taasisi mbalimbali ziwe chini ya Rais? Kwanini TAKUKURU iwe ofisi ya Rais na isiwe chini ya Waziri Mkuu… Hizi Taasisi za Ofisi ya Rais ndio zina njaa kwelikweli.. ukiona TAKUKURU inafeli maana yake Rais hana utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa.. Awamu ya nne imeshindwa kupambana na Rushwa, mnakusanya kodi hamna uwezo wa kutekeleza vitu hivi” >> Mbunge Felix Mkosamali.

Akasimama Waziri Mkuchika >> “Kwa mujibu wa kanuni inayosema Mbunge hatotumia jina la Rais kwa dhihaka katikka mjadala au kwa madhumuni ya kulishawishi Bunge.. Mkosamali ameeleza Rais hana utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa.. Kiustaarabu afute tu hiyo kauli>>

Mkosamali akaendelea >> “Nitafutaje wakati ndio hali halisi.. Juzi Katibu Mkuu amesafisha watu.. Kesi zote zikichunguzwa DPP anazifuta mbona yako wazi”>>

Akasimama Mbunge Innocent Sebba >> “Niwashukuru Mawaziri wanaohusika na Ofisi ya Rais.. Pamoja na kelele zinazopigwa hawa wenzetu tunawaita ni wapiga debe sio wasafiri.. Wanaosafiri
Baadae akapata nafasi Waziri Mark Mwandosya >> “Hoja ya leo inamzungumzia Ofisi ya juu kabisa katika nchi.. unapokizungumzia chombo hiki kipe heshima inayohitajika.. Huwezi ukamzungumzia Rais kama unavyomzungumzia Mbunge wa Rungwe“>>
 
Huyo Mzee Mwandosya naye kaanza anaanza kutoa mwelekeo kama atapitishwa atakuwa raisi wa aina gani ukishaona mtu hata kwenye ukweli anatia neno basi mtu huyo naye shiida shida kwelikweli.Naye yake yako mengi tu tunamsubiria
 
hao wapinzani lazima wabwate majimboni kwao wameshawakataa sasa wanaiona serikali kama wamewafanyia fitina
 
Huyo Mzee Mwandosya naye kaanza anaanza kutoa mwelekeo kama atapitishwa atakuwa raisi wa aina gani ukishaona mtu hata kwenye ukweli anatia neno basi mtu huyo naye shiida shida kwelikweli.Naye yake yako mengi tu tunamsubiria

Msiwe waoga hiyo siyo kulka ya mtu msemakweli; kwanini mumsubirie huyu Mzee Mwandosya kama kuna maovu yake mnayoyajua wakati kila kukicha mnamnanga Lowassa kwa ufisadi? Kama mnayo ya kuwaeleza wananchi wakati wa kuyatoa ni sasa na sio kusubiri!!
 
Ukweli haujifichi... hata watoto wadogo wanajua kuwa taasisi ya Urais kimantiki kwa sasa haina tofauti na Bongo Movies..

Wote ni waigizaji...Labda useme wengine wanafanya shootings wakiwa Ikulu...ilhali wengine wanafanyia mitaani...
 
TAKUKURU haina faida yoyote kwa umma zaidi ya kuwa dodoki la kusafisha viongozi.
 
Mkosamali yuko sahihi. kitendo cha Elimu na Afya kuifungia kwenye kiroba kimoja serikali imefanya makosa makubwa sana. Serikali isione Elimu au Afya ni Idara za kuchezea. MKOSAMALI WAAMBIE WAMESHAJISAHAU.
 
Mkosamali yuko sahihi. kitendo cha Elimu na Afya kuifungia kwenye kiroba kimoja serikali imefanya makosa makubwa sana. Serikali isione Elimu au Afya ni Idara za kuchezea. MKOSAMALI WAAMBIE WAMESHAJISAHAU.

Mkosamali na kundi lake kutoka UKAWA wakiongozwa na Tundu Lissu, nawapongeza sana kwa namna wanavyoweka unafiki pembeni na kutamka mambo ambayo yanagharimu maisha yao! Ni sisi Watanzania ndiyo tuna vichwa vigumu kuelewa sijui ni nani aliyeturoga! Maana ni wepesi wa kulaumu na kusahau! Tundu Lissu ameanzisha pambio kule bungeni "Serikali ya CCM imechoka!" linaimbwa na wadau wengi tu wanaopenda taifa hili! Bado waimbaji wa pambio hilo ndani na nje ya Bunge wameendelea kuimba lakini bado tu mnaendelea kuwa wagumu kuelewa! Ni hivi CCM ni wagumu kuelewa kwa sababu hawaelewi na wala hawashauriki! Wameshauriwa mara nyingi tu tena ushauri wa bure kabisa, badala ya kuufanyia kazi ushauri waliopewa wao wanamuona aliyetoa ushauri ndiyo tatizo! Ndiyo maana Serikali ya CCM imechoka!
 
Tatizo kubwa kwenye hili Taifa ni kuwa na viongozi wanao ongoza hili Taifa kimaarifa maarufa. Inatia aibu hata kwa mambo yako wazi mtu mwingine bila aibu anakanusha kitu ambacho kimesemwa na kuonekana kwenye medias!! Hivi hawa wanaosema katibu mkuu kiongozi hakuwasafisha mawaziri na makati wakuu walio wajibishwa na bunge ni wazima au wametokea Mirembe wakaingia bungeni?? Huu ni upuuzi na dharau kwa Watanzania na tunahitaji kufanya kitu kwenye hili Taifa. Ccm hii nchi siyo ya viongozi ni yetu wote
 
Ccm wote wameshatiwa upofu. Kama mwandosya kashindwa kuona ukweli aliosema mkosamali, halafu anataka kuwa rais basi ujue jk atakuwa afadhali *100
 
Mkosamali>> Kwanini Taasisi mbalimbali ziwe chini ya Rais? Kwanini TAKUKURU iwe ofisi ya Rais na isiwe chini ya Waziri Mkuu… Hizi Taasisi za Ofisi ya Rais ndio zina njaa kwelikweli.. ukiona TAKUKURU inafeli maana yake Rais hana utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa.. Awamu ya nne imeshindwa kupambana na Rushwa, mnakusanya kodi hamna uwezo wa kutekeleza vitu hivi" >> Mbunge Felix Mkosamali.

Akasimama Waziri Mkuchika >> "Kwa mujibu wa kanuni inayosema Mbunge hatotumia jina la Rais kwa dhihaka katikka mjadala au kwa madhumuni ya kulishawishi Bunge.. Mkosamali ameeleza Rais hana utashi wa kisiasa wa kupambana na Rushwa.. Kiustaarabu afute tu hiyo kauli>>

Mkosamali akaendelea >> "Nitafutaje wakati ndio hali halisi.. Juzi Katibu Mkuu amesafisha watu.. Kesi zote zikichunguzwa DPP anazifuta mbona yako wazi">>

Akasimama Mbunge Innocent Sebba >> "Niwashukuru Mawaziri wanaohusika na Ofisi ya Rais.. Pamoja na kelele zinazopigwa hawa wenzetu tunawaita ni wapiga debe sio wasafiri.. Wanaosafiri
Baadae akapata nafasi Waziri Mark Mwandosya >> "Hoja ya leo inamzungumzia Ofisi ya juu kabisa katika nchi.. unapokizungumzia chombo hiki kipe heshima inayohitajika.. Huwezi ukamzungumzia Rais kama unavyomzungumzia Mbunge wa Rungwe">>

Mnikulu wa IKULU alichukua fedha za escrow , swali la kujiuliza yeye kama mwangalizi wa shughuli za IKULU je hakuwagawia fedha hizo wandani wake wa IKULU? IKULU sasa si mahali patakatifu tena .
 
Huyo Mzee Mwandosya naye kaanza anaanza kutoa mwelekeo kama atapitishwa atakuwa raisi wa aina gani ukishaona mtu hata kwenye ukweli anatia neno basi mtu huyo naye shiida shida kwelikweli.Naye yake yako mengi tu tunamsubiria

Kwani Mwandosya bado anawaza Urais?, Vipi Afya yake imeimalika? au yale yale ya Lusinde aliyoyasema!!
 
Msiwe waoga hiyo siyo kulka ya mtu msemakweli; kwanini mumsubirie huyu Mzee Mwandosya kama kuna maovu yake mnayoyajua wakati kila kukicha mnamnanga Lowassa kwa ufisadi? Kama mnayo ya kuwaeleza wananchi wakati wa kuyatoa ni sasa na sio kusubiri!!

Kwel kabsa kama unao ushahdi unaoonyeasha matatizo matatizo ya mwandosya yaweke wazi tuweze kumjadiri cyo projoprojo yaan angwe angwe hazisaidii kabsa
 
Back
Top Bottom